mo dadyTV

KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

kARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

LightBlog
KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

Karibu kutangaza nasi mawasiliano 0652231836

Jumapili, 5 Machi 2017

Zaidi ya watu 100 wafariki kutokana na njaa Somalia saa 8 zilizopita

Waziri mkuu wa Somalia Hassan ali Khaire, amesema watu mia moja na kumi wamefariki kutokana na visa vinavyo husiana na ukame na baa la njaa katika eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo, katika kipindi cha saa nane zilizopita.
Ukame mbaya unaokumba Somalia unatishia maisha wa mamilioni ya watu nchini humo.
Siku ya Jumanne Rais Mohamed Abdullahi Farmajo, alitangaza ukame huo kuwa janga la kitaifa.
Umoja wa Mataifa una kadiria watu milioni tano nchini Somalia, wanahitaji msaada wa dharura na kuongeza kuwa taifa hilo ni moja kati ya mataifa manne, yaliyo katika hatari ya kukumbwa na janga la njaa.
Mataifa mengine ni Nigeria, Sudan kusini na Yemen.
Karibu watu 260,000 walifariki kutokana na baa njaa iliyokumba Somalia kuanzia mwaka 2010 na 2012.
Watu wengine 220,000 walifariki kutokana na njaa ya mwaka 1992.



Pia njaa imetangazwa katika jimbo la Unity nchini Sudan Kusini, ambayo ndiyo ya kwanza kutangazwa tangu ile ya Somalia ya mwaka 2011.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni