Malaysia imemfukuza balozi wa Korea Kaskazini kuhusiana na kifo cha Kim Jong nam ,ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea kaskazini.
Kang Chol amepewa agizo la kuondoka nchini humo katika kipindi cha saa 48, alisema waziri wa maswala ya kigeni nchini humo.
Kim Jong nam ndugu wa kambo wa Kim Jong un ,alifariki wiki tatu baada ya wanawake 2 kumpaka kemikali ya sumu usoni mwake katika uwanja wa kuala Lumpur .
Malaysia haijailaumu Korea kaskazni kwa shambulio hilo lakini kuna shauku kwamba Pyongyang ilihusika.
Balozi wa Korea Kaskazini, Bwana Kang alitangazwa persona non grata{ hatakiwa nchini humo} siku ya Jumamosi baada ya kusema kuwa taifa lake haliweza kuamini uchunguzi uliofanywa na Malaysia na kwamba uchunguzi huo ulikuwa ukiingiliwa.
Waziri wa maswala ya kigeni wa Malaysia Anifah Aman alisema katika taarifa kwamba taifa lake linataka kuombwa msamaha na balozi huyo kwa matamashi yake lakini mwanadiplomasia huyo hakuomba msamaha.
''Malaysia itajibu matusi yoyote dhidi yake ama jaribio lolote la kutaka kuiharibia sifa'',alisema bwana Anifah.
Malaysia ni miongoni mwa mataifa machache yaliokuwa na urafiki na Korea Kaskazini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni