mo dadyTV

KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

kARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

LightBlog
KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

Karibu kutangaza nasi mawasiliano 0652231836

Jumapili, 28 Mei 2017

Jumamosi, 27 Mei 2017

Rais wa Makampuni *CNBM*  kutoka Beijing CHINA *Bw. Cao Jiang Lin* amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe Paul Makonda,* jiji Dar es salaam.

Katika mazungumzo hayo, *Bw. Lin* amemuhakikisha mkuu wa mkoa *Mhe Makonda* kuwa makampuni mengi yameonyesha nia ya dhati ya kuja kuwekeza *Tanzania* na Dar es salaam ambapo tayari baadhi ya makampuni yameshaanza kuwekeza jijini *Dar es salaam.*

Katika Mazungumzo yao, *Bw. Lin* amemuahidi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe Makonda* kuwapatia *kazi vijana wa Dar es salaam zaidi ya  500* kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Ikumbukwe makampuni ya *CNBM* yako zaidi ya *500 duniani* na ndiyo makampuni yanayoongoza kwa uzalishaji wa cement na bidhaa zaidi ya *15,000 DUNIANI.*


*Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.*
*27/05/2017*
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema chama chake kinamuunga mkono Uhuru Kenyatta ktk Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

Amesema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakimuunga mkono Raila Odinga katika kuchukua nafasi ya kuiongoza Kenya.

Lakini kinyume na matarajio yao, ilipofika zamu yao mwaka 2015 rafiki yao Raila aliwageuka na kumuunga mkono adui ya Rais John Pombe Magufuri

 Mh: Mwenyekiti wa Chadema Taifa Fredrick Mboye

Jumatano, 24 Mei 2017

'Nampenda sana Profesa Muhongo, pia ni rafiki yangu,lakini kwa hili (Makontena ya Mchanga) ameshindwa kuwajibika,namuomba ajitafakari,ajitathimini ninamshauri pia aachie madaraka''
Rais Dk John Pombe Magufuli 24 Mei 2017 Saa 5.18 Asubuhi,Ikulu Dar Es Salaam.
 Rais John Pombe Magufuri

Jumanne, 23 Mei 2017

mcholaji wa nembo ya taifa almahalufu kama bibi na bwana anaishi kwa tabu na kuomba misahada   anaishi  katika hari duni tofauti na mchango wake alio utoa ktk taifa

Vijana wa chama cha mapinduzi (Ccm) ni vijana wanao lelewa katika maadili,Nidhamu na ukakamavu wa hari ya juu vijana hao hupewa fulsa ya kufundishwa juu ya nchi yao hii ni tofauti na mizingi ya vyama pinzani nchini Tanzania.
kutokana na kupewa wasaa wa kuijua vizuri nchi yao basi huwa wajasili na wasio yumbishwa na ushawishi wa vyama pinzani pia vijana hao hubishana kwa hoja na si ubishi usiokuwa na msingi
Vijana wa Ccm

Jumapili, 21 Mei 2017



Bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma limeghubikwa na mijadala mingi na ya kusisimua ikihusisha hoja nzito zinazotoka kambi za upinzani na CCM, huku pia mawaziri wa kale na wapya wakionekana kana kwamba wana ‘ligi’ yao.

Wakati aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ‘akipambana’ na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge alipochangia kuhusu suala la maji jimboni kwake, Waziri wa zamani wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye alionyesha msuli wake katika suala maji jimboni kwake.

Kitwanga alieleza kuwa yale aliyochangia kwenye bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji bungeni ni kama ali-‘beep’ ila mazito yanakuja.
Hata hivyo, Lwenge alimjibu Kitwanga kuwa kama haoni mambo Serikali ilifanya katika wilaya yake ajiondoe katika chama hicho.
“Sasa anaposema anakwenda kuhamasisha wananchi wakabomoe mtambo wa Ihelele maana yake analeta uasi au hathamini kazi iliyofanywa na chama chake,” alisema.
 

Ijumaa, 19 Mei 2017



Kwa muda wa wiki moja sasa kampuni ya Sahara Communications Limited, wamiliki wa Star TV na vyombo vingine vya habari kupitia mitandao ya kijamii wanasambaza taarifa kuwa watafanya mahojiano maalum na Mkuu wa Mkoa wa Dar ea Salaam, Paul Makonda, Jumatatu Mei 22, 2017.

Kusudio hilo la Star TV limekuja wakati kiongozi huyo akiwa amefungiwa na vyombo vya habari kwa uamuzi ulioitikiwa kwa pamoja baina ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na kuungwa mkono na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT) na taasisi nyingine za kihabari nchini. Uamuzi wa kumfungia Makonda uliotangazwa Machi 2017, ilitokana na kiongozi huyo kuvamia Kituo cha Utangazaji cha Clouds Madia, March 17, 2017 akiwa na askari wenye bunduki.

Uvamizi wa Clouds ulikuwa mwendelezo wa matukio ya RC Makonda kudhalilisha wanahabari, kutukana na kutoiheshimu taaluma ya habari. Katika tamko hilo, Makonda tulimpa masharti mepesi kurejesha uhusiano na tasnia ya habari, ambayo ni kuomba radhi waandishi wa habari kwa tukio la Clouds na matukio mengine kwa ujumla wake kama sehemu ya uungwana wa Kitanzania.

Tulisema katika tamko kwa yeyote atakayeshirikiana na Makonda naye tutamhesabu kama adui wa tasnia ya habari nchini. Kwa mantiki hiyo tunasema ikiwa Star TV wameamua kushirikiana na Makonda, basi ni wazi wameamua kwa hiyari yao wenye kujitangaza kama adui wa tasnia ya habari nchini.

Kila Mtanzania anajua jinsi ya kupambana na adui kwa namnaya kujilinda, na tasnia haitasita ku fanya hivyo. Kadhalika hivi sasa TEF tunafuatatilia kwa karibu uhusiano wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na vyombo vya habari kutokana na matukio ya mara kwa mara ya kudhalilisha wanahabari wanapokuwa kazini kwa amri yake. Matukio haya yakiendelea, tutalazimika kupitia uhusiano wa RC Gambo na vyombo vya habari nchini.

Mwisho, tunavipongeza vyombo vya habari, kwa maana ya magazeti, radio, televisheni na mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi kwa kutekeleza uamuzi wa kumfungia RC Paul Makonda kwa uaminifu uadilifu wa hali juu, licha ya vishawishi vya hapa na pale vinavyotolewa na wapambe wake.

Nguvu yetu ipo katika umoja wetu kama wanahabari. Tusiipoteze Mungu ibariki Tanzania.

Deodatusi Balile
Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania.
Mei 19, 2017
Msichana mwenye umri wa miaka 18, ‘Mangli Munda’ alazimishwa na wazazi wake kufunga ndoa na Mbwa huko nchini India, kufanya hivyo ilikuwa ni imani kufukuza roho za kishetani na mikosi inayomsonga na Mbwa huyo alitafutwa na Baba mzazi wa mrembo huyo na kufanya sherehe kubwa na kufanya vitendo vyote vinavyofanywa na bibi harusi kwa taratibu za ndoa, kwa mujibu wa Yahoo News, msichana huyo hakuwa na furaha kabisa na alieleza wazi jinsi alivyochukizwa na kitendo hicho,“Sifurahii kabisa hii ndoa coz tulilazimika kutumia pesa nyingi kwa ajili ya ya hii ndoa.
Hiyo ndiyo njia pekee tunayofanya kuondoa mikosi kwa kufanya tendo jema kwa ajili ya kijiji chetu.” Amekaririwa mama yake Munda.

Jumatatu, 15 Mei 2017

Jana tar 14/05 kulikuwa na tamasha la vijana ambalo liliandaliwa na mwenyekiti wa mtaa wa kivule Mh.Mzava tamasha hilo la hamasa kwa vijana wafanye kazi lilihudhuliwa na wazanii mbalimbali ambao walitumbuiza katika stage miongon mwao ni G love,mister A,,Buzzuki, na nk nahawa ni wasanii miongoni mwao ni G love na Buzzuki wanatuelezea walivyo kiwasha stageni na nini maon yao katika tamasha hilo

Jumapili, 7 Mei 2017

MMOJA wa wazazi ambao watoto wao wamefariki katika ajali ya gari iliyosababisha vifo vya wanafunzi 33 wa Shule ya Msingi Lucky Vincent, alikuwa miongoni mwa mashuhuda wa ajali hiyo pasipo kujua kama mtoto wake, Justine Alex, alikuwamo katika msafara wa gari hilo.
Mzazi huyo, aliyetambulika kwa jina la Lemburis Saruni, inadaiwa kuwa alishuhudia ajali hiyo akiwa kwenye gari la nyuma, huku lile lililobeba wanafunzi hao likiwa mbele.
ndugu wa karibu na Lemburis ambaye hakutaka jina lake litajwe , alisema baada ya kuona gari hilo limeanguka kwenye korongo alilazimika kushuka ili kwenda kuangalia bila kujua kama mtoto wake ni miongoni mwa waathirika wa ajali.
“Hiyo ajali imeua ndugu zangu, akiwamo mtoto wa baba yangu mdogo, na yeye leo alikuwa anakwenda Ngorongoro, alifuatana na hilo basi la wanafunzi bila kujua na kaliona likidondoka, akashuka akalifuata akakuta mwanawe ndio yupo ananing'inia mlangoni,” alisema ndugu huyo.
Alisema baada ya kumuona akiwa katika hali hiyo, alilazimika kumwondoa na kumuweka pembeni, lakini kwa bahati mbaya alikufa akiwa amemshika mkononi.
Alisema Justine alikuwa mtoto pekee wa Lemburis. Alisema mama wa Justine alifariki dunia mwaka juzi.
Mwandishi wa habari hii alijaribu kumtafuta mzazi huyo kwa njia ya simu ya kiganjani ili aweze kuelezea tukio hilo, lakini hakupatikana hewani.
Mbali na mtoto huyo, mtoa taarifa alibainisha kuwa ajali hiyo huenda ikawa imesababisha vifo vya ndugu zao wengine watano ambao walikuwapo katika msafara huo, ambao ni wanafunzi na walimu.
Chama cha mapinduzi Ccm kimetoa salamu zake za rambilambi kwa ndugu na jamaa wa wanafunzi waliopata ajali huko arusha
Barua toka kwa ccm

Chama tawala nchini Tanzania kinachoitwa Chama cha mapinduzi (CCM) huwa kina kawaida ya kipekee Barani Afrika kwa kutengeneza viongozi watakao kuja kutawala nchini humo na viongozi hao wanaoandaliwa kwa ajili ya kuja kuongoza baadae ni vijana
vijana wa ccm
Vijana hao hukuzwa kwa nidhamu ukakamavu na uwadilifu.. 
Tamaduni hii ya kuandaa vijana kuwa viongozi ni yakipekee kabisa balani Afrika na hata nchini Tanzania mmoja kati ya vijana ambao waliandaliwa vyema kuja kuwa kiongozi wa Tanzania ni Rais mstafu wa Awamu ya 4 Mh.Jakaya mlisho kikwete

Historia Fupi ya Rais mstaafu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Jakaya M. Kikwete


Asili.

Amezaliwa 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugobatarafa ya Msoga,jimbo la uchaguzi la ChalinzeWilaya ya Bagamoyomkoa wa Pwani.
Alizaliwa katika familia ya wanasiasaBabu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifuwa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya PanganiSame na Tanga.
Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwamja mzito naye, babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithiwa cheo chake.

Masomo

Miaka 1958 – 1961 akasoma Shule ya Msingi Msoga, halafu 1962 – 1965 Shule ya Kati (Middle School) Lusonga, halafu Shule ya Sekondari Kibaha akiongeza A-level huko Shule ya Sekondari Tanga.
Kuanzia mwaka 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaamakimaliza kwa kupata digrii yake mwaka 1978.
Akajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Jakaya aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzina pia wa Vijana wa TANU. Katika Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuuna pia kiongozi wa timu ya mpira. Katika UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wahalmashauri ya wanafunzi.

Kupanda ngazi katika siasa

1mwaka huu alikuwa mkulima wa Msoga. Mwaka 1988 akateuliwa kuwa mbunge nawaziri msaidizi. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/Chalinzeakirudishwa kila uchaguzi hadi mwaka 2000. Akawa waziri akipita katika wizara zamaji na fedha.
Mwaka 1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwalimu Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia nafasi Benjamin Mkapa aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawaWaziri wa Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa.
Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya rais akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za kura zote.
Kutokana na Historia Hii fupi Tunaona jinsi Rais mstafu Jakaya mrisho kikwete alivyo andaliwa vizuri kisiasa na kuja kuwa kiongozi mzuri wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania....
Napenda kushauli vyama pinzani au vyama vya kisiasa kufata mfumo huu wa kuandaa viongozi tangu wakiwa wadogo ili kuweza kuja kupata viongozi bora wa baadae