mo dadyTV

KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

kARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

LightBlog
KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

Karibu kutangaza nasi mawasiliano 0652231836

Jumatatu, 26 Juni 2017

Producer bora toka Arusha aliewai kuproduce hit song nying ikiwemo nishuke wapi ya real voice inasemekana kudaiwa kuachana na mpenzi wake aliekuwa akijulikana kwa jina la Johari na sasa hupo katika wimbi la mapenzi mazito na kigori mmoja huko arusha ambaye atukuweza kumjua jina Wawili hao wamekuwa wakioneka sehemu mbalimbali za bata...
Mo fravour
Blog yetu inaendelea kunafanya juhudi za kumtafuta Johari ili atusibitishie ameachana na Mo Flavour au la

Ijumaa, 23 Juni 2017

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amelazimika kula chakula na kunywa maji yaliyotoka kwenye mradi wa maji wa kisima kirefu uliokataliwa na wananchi kwa hofu kuwa wakinywa maji hayo watakufa na wakipikia chakula kitabadilika rangi ya njano.
Mkuu huyo akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji hicho juzi alitaka kusikiliza kero za wananchi na kufahamu kwanini wanaendelea kutumia maji ambayo siyo safi na salama ikiwa mradi upo tangu mwaka 2014 hawajawahi kuyatumia.
Matiro aliyekuwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama na viongozi wengine na baada ya kusikiliza hoja hiyo walilazimika kuyaonja na kupika chakula kwa haraka na kubainika hayana chumvi wala chakula kilichopikwa kutokuwa cha njano ndipo ilipobainika kuwa walidanganywa kwa sababu za kisiasa.

Jumatatu, 19 Juni 2017

WATANZANIA wametakiwa kutoa taarifa wanabaini uwepo wa mchele usioeleweka, baada ya kuibuka kwa taarifa ya mchele bandia wa plastiki kukamatwa Nigeria.
Msemaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudencia Simwanza alisema hayo jana .
Alisema wao sasa wana mifumo mizuri ya kudhibiti uingizwaji wa bidhaa zisizofaa na mpaka sasa mfumo huo haujabaini mchele wa aina hiyo nchini.
"Tunadhibiti na tuko makini kufuatilia wafanyabiashara wanaoingiza vitu haramu na kama huo mchele ungekuwa umeingia, tungeshajua," alisema.
Mwandishi wa habari hii alipomwuliza ikitokea umeingizwa kimagendo nchini, Watamzania watautambua vipi, Gaudencia aliwataka kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa watakapoona mchele wasiouelewa.
Mchele huo bandia ulikamatwa na Mamlaka ya Mji wa Lagos, Nigeria wiki hii, ambapo walikamata magunia 102.
Taarifa kutoka nchini humo, zilieleza kuwa uliingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu na unafanana na mchele wa kawaida, hivyo ni ngumu kuutofautisha na mchele wa kawaida.
Kutokana na kusambaa kwa kasi kwa mchele huo, huwezi kuutambua kwa haraka hadi pale unapopikwa ndipo unaweza kuona ni mchele wa plastiki. Hata hivyo baadhi ya wataalamu walisema kabla ya kuupika mchele huo ukilowekwa kwenye chombo chenye maji unaelea tofauti na halisi ambao huzama.
Hospitali ya Muhimbili imemkamata kijana aliyejifanya Daktari na kuanza kuhudumia watu idara ya benki ya damu hospitalini hapo.Msemaji wa Hospitali yaTaifa Muhimbili Aminiel Eligaesha, amesema kuwa huo ni mwendelezo wa kuwakamata vishoka ndani ya Hospitali hiyo.Picha ya Gazeti la #Mwananchi
 
Jumatano, 14 Juni 2017

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi ameendelea na juhudi za utatuzi wa migogoro ya ardhi ambayo inahusisha wananchi wenye mashamba katika maeneo ya Kinondo, Dovya na Mbopo.
Juhudi hizo zimedhihirika Leo katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa kilichohusisha wananchi pamoja na wataalam wa Mipangomiji kwa kuwaahidi wananchi hao kumaliza mgogoro hiyo ili waweze kuishi kwa amani.
Hapi amesema dira ya Wilaya ya Kinondoni ni kuhakikisha viwanja vyote vinapimwa ili kuweka mipango mizuri ya matumizi ya Ardhi itakayozuia uvamizi wa mashamba pamoja na maeneo ya wazi.
Aidha amewataka wale wote wanaomiliki maeneo hayo kuyaendeleza baada ya kufanyiwa upimaji ili kuepusha migogoro ya mipaka inayoweza kutokea.
Migogoro mingine inayoendelea kutatuliwa ni pamoja na TBA Mabwepande na Nyakasangwe ambayo kwa sasa maeneo hayo yamefikia hatua ya upimaji viwanja.
Mkuu wa wilaya ya kinondoni Ally Hapi
Rais mstaafu Dk Jakaya Mrisho kikwete amehudhuria mkutano wa kwanza wa Baraza la Wakimbizi Duniani mjini Geneva Uswisi akiwa mmoja wa wenyeviti wa baraza hilo.

Jumamosi, 10 Juni 2017

Producer bora toka arusha anaejulikana kwa jina la mo flavour baada ya mda mrefu kutuficha kuwa hana mahusiano na mwanamke yeyote leo tumepokea taarifa toka kwa papalazi mmoja na usibitisho kuwa mo Flavour ana mahusiano na bint mmoja mwenye asili ya kihind anaeitwa Johari
Johari
Mo flouvar na Johari
Papalazi huyo alituleza kuwa johari na mo flavour wanapendana sana na wanaonekana mara kwa mara wakiwa pamoja
Leo ktk ukumbi wa chek point pale kigogo fresh kulikuwa na kikao cha semina elekezi kwa viongozi wa Uvccm .Dhumuni la semina hiyo elekezi ni kutoa maelekezo kwa viongozi wapya waliochaguliwa nini chama chao kinaitaji pia kujua mipaka ya uongozi wao bila kusahau kujua maadili ya chama chao..

Mgeni rasmi katibu mkoa wa Dar es salaam
Said Yassin
Watoa mada
Mashaka Nyadhi

Frank Mang'ati 
Mwenyekiti Uvccm wilaya ya ilala
alfrd Tukiko

Alhamisi, 8 Juni 2017

Dr Ulimboka alikuwa mwenyeki wa taasisi ya Madaktari nchini Tanzania, Dr ulimboka alitisha mgomo wa madaktali nchi nzima usio na kikomo tar 24 jun 2012 kwa madai ya Serikali imekataa madai yao yote walio wasilisha katika kamati ya majadiliano iliyoundwa na waziri mkuu mstaafu Mizengo pinda.....
Wakati mgomo ukiendelea tar 27 ucku zilipatikana taarifa za kutekwa kwa Dr ulimboka na hakuna mtu alie jua alitekwa na nani na yupo wapi baada ya cku kazaa Dr ulimboka alipatikana katika msituni akiwa amelowa damu kutokana na kipigo kikali
  
Dr ulimboka

inasemekana Dr ulimboka alipata mateso makali kutoka kwa watekahi hao .

MJUE ALIE MTEKA DR ULIMBOKA
Baada ya siku kazaa kupita gazeti la mwanahalisi lilitoa taarifa za alie mteka Dr ulimboka nazo ni hizi hapa chini

Kutoka Mwanahalisi:
Waliomteka dr. Ulimboka hawa hapa
Anaitwa RAMADHANI IGHONDU, a.k.a RAMA ni afisa Usalama wa Taifa(TISS) anayefanyia kazi zake ikulu katika idara ya siasa chini ya Zoka, MwanaHALISI linaeleza. Kachero huyo (RAMA) ndiye aliekuwa akijitambulisha kama ABEID wa ikulu na alikutana na ulimboka tangu mgogoro wa kwanza wamadaktari. Rekodi katika simu ya Ulimboka 0713731610, inaonyesha Rama ndiye alikuwa mtu wa mwisho kufanya naye mawasiliano Saa 5;52 kwa kupitia simu yake (RAMA) 0713760473, muda mchache kabla ya kutekwa kwa ulimboka.
Kabla ya ULIMBOKA kutekwa, RAMA alifanya naye mazungumzo saa12:25 jioni, saa 3:29 usiku, saa 4:52, saa 5:27, saa 5:40 na mwiso ilikuwa saa 5:52 usiku na mwenye namba hiyo ndiye aliyeandaa kukutana na ULimboka usiku naye (ULIMBOKA) amethibitisha bila shaka yeyote kuitambua namba hiyo ya ABEID.
Kabla ya namba hiyo kufanya mawasiliano na Ulimboka saa 12:25 ilifanya mawasiliano na BURUANI NTILONGWA (0712359533) pia kati ya saa 2:08 na 2:24 usiku. Aitha mwandishi (KUBENEA) anasema ripoti yake inaonyesha kila muda ambao RAMA alikuwa akifanya mazungumzo na Ulimboka pia alifanya mawasiliano na MOSHI MARUNGU SHABANI (0761132663 & 0655162663), ABDALLAH KUNJA na NTILONGWA. Siku mbili kabla ya kutekwa ulimboka simu ya RAMA iliingiziwa (airtime) salio la tshs 252,849/- ambalo ni salio kubwa kuingizwa tangu mwanzo mwa mwaka huu ukizingatia tarehe 04 Mei mwaka huu simu ya Rama ilikuwa na Tshs.01. Wengine waliokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na RAMA kabla ya kutekwa Ulimboka ni; Mohamed Hassan 0655524444, Shomari Kondo 0714666304. Optat Jacob Marandu 0716611625 na Mbega Hisbert 0715222778.
Taarifa nyingine kutoka ndani ya Tiss zinasema agent RAMA, tangu tarehe 26 Juni 2012 baada ya kufanikiwa kwa jaribio la kumteka Ulimboka, RAMA aliacha kutumia simu yake hiyo. Na tarehe 01 july amekuwa akituma sms kwa namba nne tofauti kwa zaidi.
Wakati wakimtesa Ulimboka ni RAMA aliyekuwa akisisitiza kuelezwa ni nani hasa katika CHADEMA aliyemtumia. Wazo lililopo Usalama wa Taifa ni kuwa Ulimboka anatumiwa na Mnyika pamoja na Dr. Slaa. Chini ya Zoka, wanatakiwa kuangamizwa hasa wale wanao ikosoa sana serikali.
Nukuu kutoka mwanahalisi.

ushuhuda wa Dr Ulimboka
Rais Jakaya Kikwete azungumzia