mo dadyTV

KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

kARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

LightBlog
KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

Karibu kutangaza nasi mawasiliano 0652231836

Alhamisi, 9 Machi 2017

Marekani yapinga pendekezo la China kuhusu K. Kaskazini



Maafisa wa Marekani wamepinga pendekezo kwamba Korea Kaskazini itasitisha majaribio ya makombora yake na yale ya Kinyuklia iwapo Marekani itasitisha vitendo vyake katika eneo hilo.

    Idara ya maswala ya kigeni nchini humo imesema kuwa mpango huo hautasaidia huku balozi wa Umoja wa Mataifa akisema kuwa Korea Kaskazini haifikirii.
    Pendekezo hilo la China linajiri baada ya Korea kaskazini kufanya majaribio ya makombora yake manne ikiwa ni ukiukaji wa vikwazo vya kimataifa.
    Wakati huohuo, Marekani imeanza kupeleka mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora nchini Korea Kusini.
    Pia inaendela na mazoezi ya pamoja na wanajeshi wa Korea Kusini hatua inayokasirisha Korea kaskazini.
    Waziri wa maswala ya kigeni nchini China Wang Yi alisema siku ya Jumatano kwamba hali hiyo ni sawa na treni mbili zinazokaribiana kugongana ana kwa ana baada ya moja kati yazo kukataa kuipisha nyengine.
    Usitishwaji wa operesheni za kijeshi na pande zote mbili unaweza kupunguza hali ya wasiwasi na kufungua mazungumzo alisema.
    Lakini msemaji wa idara ya maswala ya kigeni nchini Marekani Mark Toner alisema kuwa hilo ni sawa na kufananisha ''tufaa na chungwa''.
    ''Kile tunachofanya kama ushirikiano wetu kujilinda na Korea Kusini ni tofauti na ukiukaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na Korea Kaskazini''.
    Lakini amesema kuwa Marekani inafaa kuangalia mbinu nyengine za kukabiliana na Korea kaskazini.
    ''Juhudi zote tulizofanya kujaribu kulishawishi taifa la Korea Kaskazini kufanya majadiliano zimegonga mwamba.
    ''Kwa hivyo tunafaa kuangalia mbinu mpya za kulishawishi taifa hilo kuona kwamba ndilo litalalofaidika''.

    Hakuna maoni:

    Chapisha Maoni