mo dadyTV

KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

kARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

LightBlog
KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

Karibu kutangaza nasi mawasiliano 0652231836

Jumapili, 19 Machi 2017

MAKONDA AWANYOOSHA SHILAWADU

kwanza naanza kwa kumpongeza mkuu wa mkoa Rc makonda kiuhalisia/ kibinadam haiwezekani mtu akakuzalilisha watu na media zikaunga mkondo kwa uzalilishwaji kwako alafu wewe ukatoa ushahidi wa kitu husika media hizohizo zikakataa kucheza, safi sana Rc paul makonda kwa ulichowafanyia shilawadu nahisi wamepata fundisho na wengine
                                          picha paul makonda

 RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU::
Makonda alikuwa ofisi za Clouds mapema kuliko kawaida yake, mpaka tukahoji jamaa ana kipindi Clouds nini maana si kwa kuja huko kila siku lakini tuitetea tukajua ni sawa kama viongozi wengine wanavyofikaga mjengoni kila siku maana nikawaida yao!

Cha ajabu siku hiyo alikaa mpaka usiku akawa anamtafuta soudy Brown na Qwisser wa SHILAWADU muda huo walikuwa bado hawajafika kazini basi akawa anazungukazunguka tu ofisi hii anatokea ile kama mfanyakazi wa Clouds.

Kwenye Mida ya Saa kumi hivi akakutana na kina Soudy pamoja na prodyuza wa kipindi wakawa wanaongea kwa uficho hivi na usiri tukajua tu ni mambo ya kawaida ya kuhitaji uprivate lakini siku ile ulikuwa unatia mashaka sana.

Kumbe Makonda alikuja na Story ya mwanamke mmoja ambaye yeye Makonda alisema huyo mwanamke amezaa na mchungaji Gwajima na ametelekeza akawa anataka arekodiwe na ubuyu uruke kwenye kipindi cha SHILAWADU.

Basi wakakubalia kwa kuwa ni habari itabidi huyo mwanamke arekodiwe na kipindi kiruke siku ya jana lakini kawaida ya Kipindi cha SHILAWADU ubuyu ukipatikana lazima kila mtu apewe Natural Justice ya kusikilizwa pande zote mbili sababu huwa ndiyo kawaida ya kipindi.

Makonda siku hiyo hiyo ya Alhamisi akamwambia Soudy ajiandae then huyo mwanamke mnayemuona kwenye video na mtoto aliletwa na wasaidizi wa Makonda ahojiwe na Soudy Brown tayari kwa kurushwa kwa kipindi.

Siku ya Ijumaa ambayo ilikuwa ni jana SHILAWADU wakamtafuta Gwajima kwa upande wake kama anaifahamu hiyo ishu na je mwanamke huyo aliyetajwa ni kweli kwasababu tunaelewa ugomvi uliopo kati ya Makonda na Gwajima isijekuwa SHILAWADU wanatumika kuwafitinisha watu vibaya!

kwa bahati mbaya Gwajima hakupatikana jana ijumaa kwa ajili ya kurekodiwa na kufanyiwa mahojiano.

SHILAWADU wakatumia busara mpaka apatikane Gwajima scene ya Dada mwenye mtoto ziende kwa pamoja na ya mchungaji Gwajima kama kawaida ya POVU inavyokuwaga.

Jana usiku sasa kumbe Makonda alikuwa anafuatilia kipindi cha SHILAWADU aone kama kile kipande kitaruka hewani wapi ndiyo akaamua kuja Clouds na magari mawili yeye mwenyewe Makonda na Watu kama nane hivi wakiwa na Bunduki aina ya SMG geti la kawaida mlinzi alifungua geti kwasababu amezoeleka Mh anakujaga mjengoni wakafunguliwa kisha wakaingia ndani.

Walipofika reception wakazuiwa kuingia ndani sababu hatuna utaratibu wa kuruhusu wageni baada ya saa Nne usiku kuingia ndani ya Ofisi kama siyo mfanyakazi wa CLOUDS.

Alipoona wanazuiwa wakatoa bunduki zao mlinzi akashurutishwa afungue mlango kwa nguvu sababu walimtishia na Silaha mlimzi akafungua mlango wakaenda naye hadi studio kipindi kilikuwa kinaendelea hewani.

Makonda akawatoa nje Soudy na Mwenzake Qwisser akawauliza kwanini video aliyowaletea haijachezwa wakaelezea utaratibu jinsi utaratibu ulivyokuwa Qwisser wakati anajielezea akapigwa mtama akaanguka chini wakavamia mitambo ya transmission kwenye traycaster wakitaka kile kipande kirushwe hewani prodyuza wa kipindi akamuambia Makonda kwanini anavunja utaratibu na kutumia nguvu na ameshapewa utaratibu akapigwa na kitako cha Bunduki mgongoni akaanguka chini bahati mbaya kipindi kilikuwa kimefika mwisho.

Wakamshurutisha Prodyuza wa SHILAWADU anaitwa Chriss awape kile kipande wakaondoka naye wakati wanaondoka Ruge alikuja na Polisi akaingia lakini tayari walikuwa wameondoka ofisini wamechukua hicho kipande cha Video ya huyo mwanamke.

Hizo video zilichukuliwa kwa nguvu na Makonda na hao watu waliokuwa na Silaha inasemekana Makonda ana timu yake wanazisambaza kwa kasi na hatujui lengo lake ni nini.

Hata mkihitaji footage za Camera zipo jinsi tukio lilivyokuwa usiku wa jana.

By MANKA MUSA
JF-Expert Member
Source JF







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni