mo dadyTV

KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

kARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

LightBlog
KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

Karibu kutangaza nasi mawasiliano 0652231836

Jumatatu, 10 Julai 2017

Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema CCM, William Ngeleja ametangaza kurejesha pesa za ESCROW, kiasi cha Tsh. mil. 40.4 alizopokea kutoka kwa James Rugemalira anayetuhumiwa katika sakata la ESCROW tarehe 12 Februari 2014. Ngeleja amewaambia wanahabari leo kuwa,tayari amerudisha TRA TSh 40.4milioni alizokuwa amepewa na mfanyabiashara James Rugemalila.

Jumatatu, 26 Juni 2017

Producer bora toka Arusha aliewai kuproduce hit song nying ikiwemo nishuke wapi ya real voice inasemekana kudaiwa kuachana na mpenzi wake aliekuwa akijulikana kwa jina la Johari na sasa hupo katika wimbi la mapenzi mazito na kigori mmoja huko arusha ambaye atukuweza kumjua jina Wawili hao wamekuwa wakioneka sehemu mbalimbali za bata...
Mo fravour
Blog yetu inaendelea kunafanya juhudi za kumtafuta Johari ili atusibitishie ameachana na Mo Flavour au la



Ijumaa, 23 Juni 2017

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amelazimika kula chakula na kunywa maji yaliyotoka kwenye mradi wa maji wa kisima kirefu uliokataliwa na wananchi kwa hofu kuwa wakinywa maji hayo watakufa na wakipikia chakula kitabadilika rangi ya njano.
Mkuu huyo akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji hicho juzi alitaka kusikiliza kero za wananchi na kufahamu kwanini wanaendelea kutumia maji ambayo siyo safi na salama ikiwa mradi upo tangu mwaka 2014 hawajawahi kuyatumia.
Matiro aliyekuwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama na viongozi wengine na baada ya kusikiliza hoja hiyo walilazimika kuyaonja na kupika chakula kwa haraka na kubainika hayana chumvi wala chakula kilichopikwa kutokuwa cha njano ndipo ilipobainika kuwa walidanganywa kwa sababu za kisiasa.

Jumatatu, 19 Juni 2017

WATANZANIA wametakiwa kutoa taarifa wanabaini uwepo wa mchele usioeleweka, baada ya kuibuka kwa taarifa ya mchele bandia wa plastiki kukamatwa Nigeria.
Msemaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudencia Simwanza alisema hayo jana .
Alisema wao sasa wana mifumo mizuri ya kudhibiti uingizwaji wa bidhaa zisizofaa na mpaka sasa mfumo huo haujabaini mchele wa aina hiyo nchini.
"Tunadhibiti na tuko makini kufuatilia wafanyabiashara wanaoingiza vitu haramu na kama huo mchele ungekuwa umeingia, tungeshajua," alisema.
Mwandishi wa habari hii alipomwuliza ikitokea umeingizwa kimagendo nchini, Watamzania watautambua vipi, Gaudencia aliwataka kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa watakapoona mchele wasiouelewa.
Mchele huo bandia ulikamatwa na Mamlaka ya Mji wa Lagos, Nigeria wiki hii, ambapo walikamata magunia 102.
Taarifa kutoka nchini humo, zilieleza kuwa uliingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu na unafanana na mchele wa kawaida, hivyo ni ngumu kuutofautisha na mchele wa kawaida.
Kutokana na kusambaa kwa kasi kwa mchele huo, huwezi kuutambua kwa haraka hadi pale unapopikwa ndipo unaweza kuona ni mchele wa plastiki. Hata hivyo baadhi ya wataalamu walisema kabla ya kuupika mchele huo ukilowekwa kwenye chombo chenye maji unaelea tofauti na halisi ambao huzama.
Hospitali ya Muhimbili imemkamata kijana aliyejifanya Daktari na kuanza kuhudumia watu idara ya benki ya damu hospitalini hapo.Msemaji wa Hospitali yaTaifa Muhimbili Aminiel Eligaesha, amesema kuwa huo ni mwendelezo wa kuwakamata vishoka ndani ya Hospitali hiyo.Picha ya Gazeti la #Mwananchi