mo dadyTV

KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

kARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

LightBlog
KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

Karibu kutangaza nasi mawasiliano 0652231836

Jumapili, 30 Oktoba 2016

Bondia wa Tanzania thomas mashali amefali dunia baada ya kuzaniwa mwizi huko kiwalani nakuweza kupigwa hadi kufa na wananchi


Siku chache baada ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kubatilisha hukumu ya Kifo na kuwa kifungo cha maisha jela, Umoja wa Mataifa umepongeza maamuzi ya Kenya juu ya kufuta adhabu ya kifo kwa maelfu ya watu waliokuwa wakisubiri kutekelezwa hukumu hiyo dhidi yao.


Kwa mujibu wa msemaji wa wa idara ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Ravina Shamdasani, amesema hatua hiyo ya serikali ya Kenya ni ya kupongezwa, yenye kutia matumaini na inayofaa kufuatwa na nchi nyingine. Ravina amesema anaamini kuwa serikali ya Kenya itafanya mikakati ili kuhakikisha kuwa hukumu hiyo inafutwa kabisa kwa misingi ya sheria na katiba.
                                                                  wafungwa wa kenya                                                                  

Rais Uhuru Kenyatta, Jumatatu iliyopita alibadili hukumu zote za kifo katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki na kuzifanya kuwa kifungo cha maisha jela. Hatua hiyo imewaondolea adhabu ya kifo wafungwa 2,747 katika nchi hiyo ambayo haijamyonga mfungwa yeyote aliyehukumiwa kifo kwa kipindi cha miaka 30 mpaka sasa.

Kupunguzwa adhabu ya kifo kwa idadi kubwa ya wafungwa kulifanyika mara ya mwisho nchini Kenya mwaka 2009 wakati wa utawala wa Rais mtaafu Mwai Kibaki. Ripoti zimearifu kuwa, hukumu ya kifo ilitekelezwa mara ya mwisho nchini Kenya mwaka 1987.
Ni habari iliyo njema kwa muziki wa Tanzania pale unapoona mwimbaji wake anaalikwa kwenda kutumbuiza kwenye taifa ambalo sio taifa linalotumia lugha ya Kiswahili lakini muziki wa bongofleva umeweza kupenya.

Mwimbaji Diamond Platnumz wa Tanzania alialikwa kwenda kutumbuiza Malawi Ijumaa ya weekend hii na hata yeye mwenyewe amefurahishwa na mwitikio wa Malawi kwenye muziki wake.

Diamond ameandika ‘Licha ya Mvua kunyesha na kuharibu stage na system yote muziki lakini mliamua kuvumilia na kunisubiria kuanzia usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi nilipopanda na kuanza show yangu…

Imefanya niwapende na kuwathamini kuliko mliyofikiria MALAWI…shukran sana kwa mapenzi yenu kwangu, natumai Show mliifurahia…tukutane tena wakati mwingine……NIGERIA see you this weeknd‘ – Diamond
October 30 2016 mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania bara klabu ya Dar es Salaam Young Africans walicheza mchezo wao wa 12 wa Ligi Kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mbao FC ya Mwanza, Yanga katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Uhuru walifanikiwa kuibuna ushindi wa goli 3-0, magoli yakifungwa na Vincent Bossou dakika ya 49 na Amissi Tambwe dakika ya 75 huku goli moja kipa wa Mbao akijifunga.

Ijumaa, 28 Oktoba 2016


Wananchi wa Afrika Kusini wameweka video na picha katika mitandao ya kijamii, ikimuonesha Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma, alilala katikati ya Hotuba ya saa moja na dakika 14 iliyokuwa ikisomwa na waziri wa fedha Pravin Gordhan, kamera zilimnasa Rais Jacob Zuma akiwa amelala,usingizi mzito.

A patient has collapsed and died at Bungoma County Referral Hospital after waiting on the queue to be treated for over four hours.

Witnesses told Nation.co.ke that David Wekesa Kibui arrived at the hospital shortly after 8am in the company of his wife Emily and proceeded straight to a queue as they waited to be attended to.
But four hours later, witnesses say, he had not been attended to.

According to his wife, they had rushed him to the facility after he developed complications while at home.

“It is sad that this has happened,” she said.
The death has sparked demonstrations at the hospital, with residents demanding answers.

They have accused doctors and nurses of negligence.

Lady Justice Philomena Mwilu and Justice Isaac Lenaola have been sworn in as the Deputy Chief Justice and Judge of the Supreme Court of Kenya, respectively.

The two took their oaths of office before Chief Registrar of Judiciary Anne Atieno Amadi on Friday at State House, Nairobi.

Congratulating the new Deputy Chief Justice and Justice Lenaola after witnessing the swearing-in, President Kenyatta said he looked forward to working with the judiciary in serving Kenyans.

“I just want to reiterate, once again, that at the end of the day we serve the same people," the President said on Friday.

"Therefore, we need  complement each other in discharging our mandates to the people. We are not in competition."

The President assured the judiciary of his support to enable it discharge its duties effectively.

Chief Justice David Maraga, Attorney-General Githu Muigai, Foreign Affairs Cabinet Secretary Amina Mohamed, and Chief of Staff and Head of Public Service Joseph Kinyua, among other senior government officials, attended the brief ceremony.

Jana October 27 2016 iliripotiwa taarifa ya mwanaume mmoja kujaribu mshambulia afisa wa usalama karibu na ubalozi wa Marekani nchini Kenya kwa kisu, kisa hicho kimefanya ubalozi wa Marekani nchini Kenya leo October 28 2016 kutangaza kufungwa kwa muda kwa ubalozi huo.

Mwanamume aliyejaribu kumshambulia afisa wa usalama  kwa kupigwa risasi, Imeeelezwa hakuna afisa yeyote wa ubalozi huo aliyeathiriwa na kisa hicho.

Leo October 28 2016 Taarifa zilizotolewa kwenye tovuti ya ubalozi imesema ……..>>>Ubalozi utafungwa October 28 2016 na huduma zote za kibalozi zimesitishwa, lakini huduma za kibalozi za dharura kwa raia wa Marekani zitaendelea kutolewa’

Jumanne, 25 Oktoba 2016

Ikiwa leo ni October 25, 2016, Rais John Pombe Magufuli anatimiza mwaka mmoja tangu alipopigiwa Kura na wananchi wa Tanzania na kumchagua kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jarida linalofanyia tafiti watu maarufu na shughuli wanazozifanya la Forbes, limetangaza watu wanaowania tuzo ya Mtu Maarufu wa Mwaka.

Forbes wamemtaja Rais Magufuli kama kiongozi ambaye amefanikiwa kuongeza kiwango cha uchumi wa nchi yake huku akishindana na watu wengine kama Michael Le Roux ambaye ni muanzilishi wa Capitec Bank nchini Afrika Kusini, Benki ambazo zimeonekana kuwa rahisi zaidi kutumika na wananchi wa Afrika Kusini.
Wengine ni Thuli Madonsela, Ameenah Gulib pamoja na watu wa Rwanda.

Anachuana na watu wengine wanne wakiwemo: Rais wa Mauritania, Ameenah Gulib, Mwanzilishi wa Capitec Bank, Michiel Le Roux na Thuli Madonsela wa Afrika Kusini pamoja na watu wa Rwanda. Tuzo hii iliwahi kutolewa pia kwa mtanzania Mohamed Dewji mwaka 2015.
Mtu wangu unaruhusiwa kumpigia kura ya ushindi Rais Magufuli kupitia Hapa. Kumbuka mwisho wa kupiga Kura ni November 17, 2016 na tuzo hiyo itatolewa Nairobi Kenya.

Jumatatu, 24 Oktoba 2016

Nafahamu kuna watu wangu ni wapenzi wa kufuatilia updates za wasanii wa nje ya nchi nikizungumzia mastaa kama Rihanna, Kanye West, Justin Bieber, Beyonce na wengineo wengi, pia katika list rappers bora wa Marekani uwezi kuacha kumtaja Drake ambae ameingia kwenye headline na album yake ya awali ya ‘Views’.

Good news kwa mashabiki wa Rapper Drake wakae mkao wa kula baada ya Rapper huyu kutangaza kuachia album nyingine tena  ifikapo December 2016 itakayobeba jina la ‘More life’  na tayari ameshaachia nyimbo 4 katika hii album leo  Oct 24 2016.

Staa huyu aliongea maneno haya akiwa anahost show ya Radio ya Apple Beats 1, OVO Sound, na haya ndio maneno aliyoyaongea..
‘Nataka niwape mkusanyiko wa nyimbo ambazo mtazisikiliza kwenye maisha yenu yote,kwahiyo hii playlist ya More life kama nilivyosema kwamba itatoka December’ Drake

Baada ya headlines za muda mrefu zilizoanza toka October 10 2016 kuhusu hatma ya kocha mkuu wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans Hans van Pluijm kuwa anakaribia kufutwa kazi na nafasi yake kurithiwa na kocha wa Zesco United George Lwandamina.

Jioni ya October 24 2016 taarifa za kujiuzulu kocha huyo zimesambaa katika mitandao ya kijamii, huku wengi wakishangazwa na maamuzi ya kocha huyo kutangaza kujiuzulu, Hans amejiuzulu kufuatia kusikia ujio wa kocha wa Zesco United George Lwandamina ambaye inaaminika amekuja kuchukua nafasi yake.

Inadaiwa kuwa kilichosababisha viongozi wa Yanga kuwa katika mpango wa kumfuta kazi kocha Hans ni kutokana na kukataa kumrudisha kikosini Mrisho Ngassa aliyekuwa amevunja mkataba na Free State ya Afrika Kusini, Hans aliona hakuna haja ya kumrudisha Ngassa wakati kuna Deus Kaseke, Juma Mahadhi na Simon Msuva.

Najua kuna watu wangu ni mashabiki wa staa wa muziki wa RnB na Pop mwenye asili ya Canada, Justin Bieber amezikamata headlines baada ya kutupa mic chini akiwa anaperfom kwenye stage za show ya Manchester usiku wa Oct 23 2016 na kuondoka jukwaani hapo.

Imetajwa na kituo kikubwa cha habari cha Enews cha Marekani kuwa mashabiki kwenye show hiyo walikuwa wakipiga kelele za shangwe kupita kiasi na kumkera staa huyo ambapo alidai kuwa anataka aongee nao badala yake zinasikika kelele ndipo akamua kuchukua uwamuzi huo.

Enews waliongezea kuwa Justin alishawaonya mara ya kwanza mashabiki wasipige kelele wakati anaongea nao lakini hawakusikia na haya ndiyo yalikuwa maneno ya Justin…..

>>>’Nashukuru sana kwa upendo wenu mnao uonyesha kwangu, hizi kelele tafadhali naomba ziachwe ninashukuru tena lakini sidhani kama ni lazima kwenu kushangilia wakati naongea kwasababu najisikia kama nataka kuunganishwa na ninyi’  –Justin Bieber 

Nimekuwekea hapa chini video mtu wangu jinsi Justin alivyotupa Mic nakuondoka kwenye stage hiyo

Jumapili, 23 Oktoba 2016

Mabingwa wa soka barani Ulaya klabu ya Real Madrid wamechupa hadi katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi ya nchini Hispania baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Athletic Bilbao.
Karim Benzema alitangulia kuzisalimia nyavu za Bilbao katika 7, lakini dakika 19 baadae Sabin Merino aliisawazishia timu yake ambayo ilikua ugenini Santiago Beranabeu usiku wa kuamkia hii leo.
Alvaro Morata, ambaye jana alikua akisheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kufikisha umri wa miaka 24 alifunga bao la ushindi kwa Real Madrid katika dakika ya 84.
Kwa ushindi huo Real Madrid wamekwea katika kilele cha msimamo wa ligi ya La Liga kwa kufikisha point 21, wakifuatiwa na Sevilla CF wenye point 20 na nafasi ya tatu ikishi FC Barcelona wenye point 19.
Michezo mingine ya ligi hiyo iliyochezwa jana:
Celta Vigo 4 – 1 Deportivo La Coruna
Sevilla 1 – 0 Atletico Madrid
Malaga 4 – 0 Leganes
Villarreal 2 – 1 Las Palmas

Wakati Watanzania wengi macho na masikio yetu tukiwa tumeyaelekeza kwenye utoaji wa tuzo za MTVMama ambazo zimetolewa Afrika Kusini lakini usiku huo huo wa Oct 22 kuamkia Oct 23 nchini Marekani kulikua pia kukitolewa tuzo ambazo Watanzania wenzetu pia walishiriki.
 Tuzo ambazo zilitolewa marekani zinajulikana kama African Entertainment Awards Usa 2016 (AEA) kitu kizuri na kikubwa ni kwamba Watanzania wenzetu wameshinda pia kwenye tuzo hizo kwenye baadhi ya vipengele.
Kipengele cha Msanii bora anaechipukia kashinda Harmonize,Kipengele cha wimbo bora wa kushirikiana/kushirikishwa umeshinda wimbo wa Zigo wa AY,Kipengele cha DJ Bora ni Dj D Ommy na msanii bora wa kiume kashinda Diamond Platnumz.
Tuzo aliyoshinda Harmonize alikua anashindana na Tekno Miles,Ziza Bafana,Ayo Jay,Missy Bk,Jay Oliver,Den G,Togar  Howard na Ziza Bafana.Tuzo aliyoshinda AY wimbo bora wa kushirikiana alikua akishinda na Nagharamia ya Christian Bella na Alikiba,Woju ya Kiss Daniel akiwa kamshirikisha Davido na Tiwa Savage,Pimpina ya Obrafour akiwa kamshrikisha Bisa Kdei,Porque te amo ya To Semedo akiwa kamshirikisha Boss Ac na wimbo wa Nagode wa Yemi Alade akiwa kamshirikisha Selebobo.
Tuzo aliyoshinda Dj D Ommy alikua akishinda na Dj Tunez,Dj Van,Dj Mensah,Dj Brazao,Dj BossMan na Dj Jimmy Jatt,tuzo ya msanii bora wa kiume aliyoshinda Diamond kipengele hicho alikua na Eddy Kenzo,Wizkid,Mc Galaxy,Nelson freitas,Coreon Du na Master jake.


JIACHIE MUSIC FEATIVAL/Inakuletea/SHAMSILA & RAMSEE/ Ndani ya AUSTRALIA GREEN GARDEN kwa aloyce (maji ya chai ) Kingilio cha 5000/= Getini Lakini kwa Wakala wetu unanunua 3000/=
 Tarehe 19/11/2016 MUDA SAA 7:00 usiku
 Tiketi zinapatikana kwa Wakala . MSUYA SHOP (Kambi ya pili ) MEKI STATIONARY (Njia ngombe stand ) RAS M-PESA (Maji ya chai) KIMARIO SHOP (Maji mpya ) ANORLD SHOP (Sabato stand ) KWA KIBONGE CENTER (Imbaseni Umoja ) Wakisindikizwa na Emma Masai / Ras D / Bad Bero / Wakalizama / More flavour / D stanza na wengine kibao ....... Pia itakuwa birthday party ya Shamsila @shamsila1@iam_hassanmushi@shamsilatz@Designedby Willie Wolfgang
Muswada wa Huduma za Habari (Media Services bill 2016) ni HATARI

Serikali ya awamu ya Tano imewasilisha Bungeni Muswada wa Sheria kutunga Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari. Muswada wa Sheria hiyo sasa upo mbele ya kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kuchambuliwa na kisha kuwasilishwa Bungeni. 

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kanuni ya 84 Kamati ya Bunge inawajibika kuutangaza muswada na kupokea maoni ya wadau mbalimbali.

Kwa hakika wadau wa muswada huu ni wananchi Kwa muda mrefu sana Waandishi wa habari na wanazuoni mbalimbali wamekuwa wakitaka kuwepo na sheria ya kusimamia tasnia ya habari. Ninaambiwa kuwa juhudi za kutunga sheria hii ni mchakato wa zaidi ya miaka 20, tangu mwaka 1993 ambapo muswada wa kusajili waandishi wa habari uliondolewa Bungeni baada ya kuwasilishwa na Dr. William Shija wakati ule akiwa Waziri wa Wizara ya Habari na Utangazaji, ambaye sasa ni marehemu. wote kwani haki ya kupata habari ni haki ya kikatiba. Hata hivyo, waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari na mitambo ya kuchapisha magazeti na majarida ni makundi yatakayoathirika moja kwa moja na muswada huu utakapokuwa sheria.
  Hata hivyo, muswada unapelekwa mbio na mwenyekiti wa Kamati katishia kuwa iwapo wadau hawatatoa maoni, Kamati yake itaendelea na kazi zake za kutunga sheria.

Vile vile kumekuwa na kilio kikubwa cha vyombo vya habari kufungiwa kwa kutumia Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ambayo inampa mamlaka makubwa sana waziri wa Habari. Wananchi wengi na wapenda demokrasia walitarajia kwamba sheria mpya ingeweza kuondoa sheria kandamizi na kuweka uhuru wa vyombo vya habari ipasavyo. Hicho sicho kilicholetwa na Serikali.

Muswada uliopo mbele ya kamati ya Bunge unatoa tafsiri pana sana ya vyombo vya habari. Sehemu ya 3 ya Muswada inatamka chombo cha habari ni pamoja na gazeti, kituo cha radio na televisheni ikiwemo mitandao ya kijamii (online platforms). Muswada unatamka kuwa ni lazima "media house" iwe na leseni maalumu kwa ajili kufanya kazi na waandishi wa chombo hicho ni lazima waandikishwe kwenye chombo kiitwacho Accreditation Board (Bodi ya Ithibati).

Iwapo sheria hii itatungwa maana yake ni kwamba mtandao kama wa jamiiforums utapaswa kuandikishwa na watu wote wanaotoa maoni yao kwenye mtandao huo lazima wawe na ithibati! Haitaishia hapo, bali hata blogs nk zitapaswa kuandikishwa kama ilivyo magazeti. Hatua hii itaminya sana uhuru wa watu kupata habari na kupashana habari. Hata uhuru wa kujieleza utaminywa sana kupitia mitandao ya kijamii.

Muswada unataka kuwepo na sheria ya Serikali kuamua vyombo vya habari viandike nini na vitanagze nini. Sehemu ya 7(1)(b)(iv) inatamka wazi kwamba Waziri anaweza kuagiza chombo chochote cha habari cha binafsi kutangaza habari Fulani au masuala Fulani yenye umuhimu kwa Taifa.

Itakumbukwa kwamba muswada uliopita ambao ulikataliwa ulitaka ifikapo saa mbili usiku televisheni na radio zote ziungane na TBC kutangaza taarifa ya habari. Kifungu hiki ndio kitatumika kufanya suala hilo kwa amri ya Waziri. Kifungu hiki pia kinampa Waziri wa Habari mamlaka ya kuelekeza chombo cha habari kutotoa habari Fulani kwa utashi wa Waziri. Ni dhahiri kuwa huu ni ukiukwaji mkubwa sana wa uhuru wa habari na kuwa kikwazo kikubwa kwa kazi za waandishi.

Kwa kutumia kifungu hiki Waziri wa Habari anaweza kuagiza magazeti yote yasiandike habari za IPTL Tegeta Escrow na Waziri atakuwa ndani ya sheria.

Muswada pia unampa Waziri wa Habari mamlaka ya kutoa Masharti ya Kazi za vyombo vya habari (Terms and Conditions). Hii inatia nguvu kifungu hicho hapo juu kuhusu maelekezo ya habari za kutolewa na kutotolewa na vyombo vya habari.

Muswada huu umerudisha vifungu vyote kandamizi vilivyopo kwenye sheria ya magazeti ya mwaka 1976. Kwa mfano kifungu cha 54-56 kinampa Waziri haki ya kutamka kwamba gazeti Fulani au kitabu Fulani kisisambazwe nchini au kuzalishwa nchini.

Kwenye masuala mengine Mkurugenzi wa Habari Maelezo na Jeshi la Polisi linaweza kuingia kwa nguvu na kuchukua mitambo inayozalisha magazeti kwa sababu tu gazeti hilo limechapisha habari ambayo kwa maoni ya Serikali ni habari za kichochezi.

Muswada umetafsiri uchochezi kuwa ni pamoja na kuandika au kutangaza mambo ambayo yanaweza kutafsiriwa kuwa yanaleta chuki ya wananchi dhidi ya Serikali. Kwa kutumia kifungu hiki, mbunge wa upinzani akihutubia na kuonyesha ufisadi Serikalini, sheria hii inaweza kutumika kufuta vyombo vya habari vilivyoandika au kutangaza habari hiyo.

Kwa ufupi, huu ni muswada mbaya kuliko sheria ya magazeti ya sasa. Huu muswada unairudisha nchi nyuma katika juhudi za kujenga Taifa lenye Haki na wajibu. Ni sheria kandamizi ambazo kama Jaji Francis Nyalali angekuwa hai angeijumuisha katika sheria 40 kandamizi.


Serikali ya awamu ya Tano imeamua kujenga Taifa lenye giza. Rais Magufuli ameamua kukataa kata kata kuhojiwa na kukosolewa kwa kuhakikisha kuwa anavibana vyombo vya habari nchini.

Nilipata kusema huko nyuma kwamba, Serikali ikishamaliza kuvibana vyama vya upinzani itavibana vyombo vya habari. Utabiri ule umetimia kupitia sheria ya huduma za habari inayoelekea kutungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
  Oktoba 20, 2016
 Dodoma

Jumamosi, 22 Oktoba 2016

Ikiwa mwaka 2016 Tanzania imeandika historia ya kutoka kapa kwenye tuzo za MTV MAMA 2016 zilizotolewa 22 October 2016 kwenye ukumbi wa Ticket Pro Dome Johannesburg Afrika Kusini.

 Sasa kundi la Navy Kenzo  lililokuwa likiwania tuzo ya Best Group limefunguka kuhusu Tanzania kukosa tuzo hizo na kuyaongea haya>>>>Kwanza  kukosa tuzo ni kitu cha kawaida pia kuchaguliwa kuwania tuzo hizo ni mshindi ninachowaomba mashabiki na watanzania wasikate tamaa waendelee na jitihada za  kura kupiga kwa wingi pale Tanzania inapowakilishwa na msanii kwahiyo wasikate tamaa’

Unaweza ukabonyeza play kuwatazama Navy Kenzo wakizungumzia Tanzania kukosa tuzo za MTV MAMA 2016
Utoaji wa tuzo za MTV Mama 2016 zinazoandaliwa na kituo cha TV cha MTV Base Africa ulikamilika usiku wa October 22 2016 Johannesburg Afrika Kusini, msanii wa Bongofleva Diamond Platnumz alikuwa ni mmoja kati ya wasanii wa Tanzania waliokuwa nominated kuwania tuzo hizo.

Diamond alikuwa kateuliwa kuwania tuzo mbili za msanii bora wa mwaka na msanii bora wa kiume, tuzo ambazo zote alishinda Wizkid wa Nigeria, muda mchache baada ya tuzo kumalizika Diamond Platnumz alitumia account yake ya Instagram kuwashukuru wote na kuwapongeza washindi akioneshwa kukubali matokeo.

“Shukran sana sana kwa Kura na support Kubwa mlionipa na mnayoendelea kunipa…. pia S/O kwa my fellow Tanzanian Artist wote waliobahatika kuchaguliwa… Kuingia tunwengi kwenye MtvAwards ni Ushindi tosha kwa Tanzania…ila wanna congrats my brothers @sautisol for the Best Group award… my hommie @jahprayzah and@wizkidayo ya’ll deserve the Trophies….
Jeshi la Polisi mkoani Tanga kwa kushirikiana na kitengo cha operesheni na mafunzo kutoka makao makuu ya jeshi hilo   Dar es Salaam, limewaua watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi   walipojibizana kwa risasi. Wakati wa tukio hilo  Oktoba 18 mwaka huu

Alhamisi, 20 Oktoba 2016

Mimi mmiliki wa blog hii itwayo (Mo DadyTv => Mohamedydady1.blogsport.com) napenda kuwa kalibisha ktk blog yangu hii nina imani mtafalijika na kupata habari na matukio ambayo yanaendelea hapa Tanzania na sehemu nyinginezo    

                                                                                                     karibuni by
                                                                                               Mohamedydady1@gmail.com
Serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam, imewataka wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutosaini fedha za malipo ya mkopo wa kujikimu hadi hapo serikali itakapokuja na majibu.

Rais wa serikali hiyo Erasmi Leon, akitoa msimamo wa Serikali ya wanafunzi wa UDSM amesema wanapinga mfumo mpya wa HESLB ambao unawapa mkopo wanafunzi kulingana na daraja na kwamba wanafunzi wa mwaka wa kwanza hawatasaini fedha hizo mpaka pale kasoro hiyo itakaporekebishwa.

Imebainika kwamba,utaratibu mpya wa kutoa fedha za kujikimu kwa mwanafunzi kulingana na asilimia ya mkopo, ulioanzishwa na serikali mwaka huu wa masomo,umesababisha baadhi ya wanafunzi kupewa Sh. 350/= kama fedha ya kujikimu kwa siku, tofauti na mwaka jana ambapo wanafunzi wote wenye mikopo walikuwa wakipewa Sh. 8,500/= kwa siku.

Erasmi amesema wana kila sababu ya kusikilizwa na wakinyimwa nafasi watachukua hatua nyingine zaidi.
Benchi la ufundi Simba limemrudisha katika kikosi cha kwanza mshambuliaji Laudit Mavugo katika pambano la leo ligi kuu dhidi ya Mbao FC.
Mavugo alianzia benchi katika michezo miwili mfululizo iiliyopita dhidi ya Mbeya City na Kagera Sugar ambayo mshambuliaji mwenzake, Frederic Blagnon alipewa nafasi ya kwanza.
Kikosi kamili: Vicent Angban, Janvier Bokungu, Mohamed Hussein, Juuko Murshid, Method Mwanjale, Jonas Mkude, Ramadhan Kichuya, Mzamiru Yassin, Shiza Kichuya, Ibrahim Ajib, Mwinyi Kazimoto.
Akiba: Manyika Jr. Andi Banda, Said Ndemla, Novalty Lufunga, Emmanuel Simwanza, Mohamed Ibrahim, Frederic Blagnon.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe amelaani vikali tabia ya wakuu wa wilaya na mikoa nchini kuingilia mamlaka zisizo zao.

 

 Kiongozi huyo alikuwa alikuwa akizungumza na wanahabari mjini Arusha mara baada ya kuhudhuria kesi ya Rufaa ya aliyekuwa mbunge wa Longido Onesmo Ole Nangole.

 Kiongozi huyo wa upinzani bungeni ameonya na kulaani tabia ya mkuu wa mkoa wa Arusha akishirikiana na wakuu wake wa wilaya kudhalilisha madiwani wa Chadema bila sababu.

 Mwenyekiti huyo amesema viongozi hao wa kuteuliwa wamekuwa wakitengua maamuzi ya vikao halali vya mabaraza vya madiwani kihuni na bila sababu za msingi ati kwa vile tu mabaraza hayo yanaongozwa na Chadema.

 Mwenyekiti huyo amesema posho ambazo zinalipwa madiwani zilipitishwa na Baraza la madiwani wa CCM wakitaka kubadilisha posho hizo Mkuregenzi wa Jiji la Arusha anatakiwa kuwapatia madiwani waraka unatakiwa kutoka ofisi ya Tamisemi.

 Kiongozi huyo mkuu wa upinzani nchini ameagiza wanasheria wa chama kuchukua hatua mara moja dhidi ya wakuu wa mikoa na wilaya wanaofanya vitendo vinavyokiuka maadili ya kazi zao.