Karibu kutangaza nasi mawasiliano 0652231836
Jumatano, 29 Machi 2017
Jumanne, 28 Machi 2017
kimbunga kikali kinatarajiwa kupiga pwani ya Australia ya Queensland muda mfupi pamoja na upepo mkali na mvua kubwa
Maelfu ya wakazi wameondolewa kutoka miji ya pwani, na kuacha nyumba zao zikijaa maji.
Gavana wa Queensland, Annastacia Palaszczuk, amesema kwa sasa watu wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa na watu hawapaswi kutembea hovyo.
Wafanyakazi elfu mbili wa dharura wanasubiri na kujiandaa kufika katika eneo hilo kutoa msaada kwa kadri itakavyohitajika.
Taarifa za wataalam wa mambo ya hali ya hewa wanasema upepo unatarajiwa kuvuma kwa kilomita 280 kwa saa moja.

Serikali ya Yemen imesema watu 11 waliuawa katika shambulio la kujitoa muhanga kwenye uwanja mmoja Kusini mwa nchi hiyo.
Maofisa wanasema kuwa gari dogo likiwa na vilipuzi, liliendeshwa mpaka kwenye uwanja wa serikali wa al-Houta uliokuwa na mkusanyiko wa watu.
Baadhi ya watu waliokuwa wamevalia mavazi ya kijeshi walitoka kwenye gari hilo na kuanza kushambulia raia na kisha bomu kwenye gari hilo lililipuka.
Shambulizi hili linatajwa kufanywa na kundi la Islamic State ambalo mpaka sasa hawajatoa tamko lolote.

Jumatatu, 27 Machi 2017
Baraza la Sanaa ka Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo ‘WAPO’ uliombwa na msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego kutumika kwa namna yoyote ile.
Kwa mujibu wa BASATA kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kusimami kazi za Sanaa na mamlaka za kishirika kuhakikisha yote yafanyikayo katika tasnia ya Sanaa hayaachi taifa na wasanii katika hali sizizo salama.
Katika kutekeleza majukumu haya, Baraza linahakikisha linalinda maadili miongoni mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi zozote za sanaa.
Kwa muda huu, BASATA linawakumbusha wasanii na wadau wote wa kazi za sanaa kuzingatia ubunifu wa hali ya juu kufanya kazi za Sanaa, hata kufikisha jumbe mbalimbali za kufundisha, kuelemisha, kuburudisha hata kuonya.
Baraza linawaonya wale wote wanatumia kazi zilizopigwa marufuku, ikumbukwe kuwa kutumia kazi zilizopigwa marufuku ni ukiukwaji wa sheria za nchi, hatua kali zitachukuliwa juu yao.

Maelfu ya raia wamekusanyika katika maeneo tofauti nchini Urusi
wakiandamana kupinga kile wanachodai matumizi mabaya ya fedha za umma.
Mkusanyiko mkubwa upo katika mji wa Moscow ambapo shinikizo ni kumtaka waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev kujiuzulu.
Wanaharakati wanasema kuwa hadi sasa watu 800 wanashikiliwa na Polisi.
Maandamano haya yanatajwa kuwa ni makubwa zaidi ya yale yaliyowahi kutokea nchini Urusi kwa miaka mingi, ambapo wanadai kuwa waziri mkuu wao Dmitry Medvedev amekuwa akutumia fedha za umma
katika mambo yake binafsi kwa kujenga majumba kifahari, kununua boti za kifahari, mashamba ya mvinyo na jumba la kufugia bata.
Katika viunga vya Pushkin mjini Moscow, kuna kundi kubwa la waandamanaji waliokusanyika, mmoja wao amesema kuwa fedha za serikali zinaibiwa.
Marekani imeilaumu Urusi kwa hatua yake ya kuwashikilia mamia ya waandamaji kwa madai kuwa wanavuja haki dhidi ya maandamano ya amani kwa mujibu wa haki za binadamu.

Waendesha mashtaka wamesema wataomba idhini ya kumkamata aliyekuwa rais
wa taifa hilo Park Geun-hye, kwa mchango wake katika kashfa ya ulaji
rushwa nchini humo.
Alipoteza kinga ya rais dhidi ya kfuunguliwa mashtaka mapema mwezi huu na akaondolewa rasmi madarakani baada ya mahakama ya kikatiba kudumisha uamuzi wa bunge wa kumng'oa madarakani.
Bi Park anatuhumiwa kumruhusu rafiki yake wa karibu Choi Soon-sil kudai pesa kwa lazima kutoka kwa kampuni kubwakubwa. Bi Park amekanusha madai hayo.
Rais huyo wa zamani aliomba radhi kwa umma wiki iliyopita, kabla ya kuhojiwa na maafisa wa mashtaka kwa saa 14.
Waendeshaji mashtaka walisema Jumatatu kwamba "wameamua kwamba ni vyema, kwa kufuata sheria na maadili nchini humo, kuomba kibali cha kumkamata".
Wanasema ushahidi, ambao unapatikana katika diski za kompyuta huenda ukaharibiwa iwapo Bi Park hatakamatwa.
Bi Choi amefunguliwa mashtaka ya ulaji rushwa na tayari kesi dhidi yake imeanza.
Park aling'olewa vipi madarakani?
Bi Park aliondolewa madarakani kutokana na uhusiano wake wa karibu na Bi Choi.
Bi Choi anatuhumiwa kutumia uhusiano wake na rais huyo kushinikiza kampuni kutoa mamilioni ya dola kama mchango kwa nyakfu za kusaidia jamii ambazo alikuwa anazisimamia.
Kaimu mkuu wa kampuni kubwa ya vifaa vya kielektroniki ya Samsung, Lee Jae-yong, alikamatwa kuhusiana na kashfa hiyo.
Bi Park, 65, anadaiwa kuhusika moja kwa moja katika hili, na kwamba alimruhusu Bi Choi uhuru wa kiwango kisichokubalika wa kufikia nyaraka rasmi za serika

Baada ya jeshi la Polisi mkoan Morogoro kuthibitisha kukamatwa kwa msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego sasa basi taarifa iliyonifikia ni kwamba tayari msanii huyo ameshafikishwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam jioni hii.
Sasa miongoni mwa mawakili walioguswa na kukamatwa kwa msanii huyo ni wakili Peter Kibatala ambae kupitia ukurasa wake wa instagram aliyaandika haya….>>>Nay wa Mitego amefikishwa Central Police Station, Dar es Salaam yuko salama na imara amekula pia. Kwa kuwa amefika jioni sana; hakuna kinachoweza kufanyika leo Wakili Faraji Mangula alifika pale, na kesho tutapigana afikishwe Mahakamani au apewe dhamana‘- Peter Kibatala

Jumapili, 26 Machi 2017
Jumamosi, 25 Machi 2017
Aliyekuwa mshauri wa maswala ya kiusalama wa rais wa Marekani Donald
Trump ,Michael Flynn alizungumza kuhusu kumuondoa kiongozi wa dini aliye
mafichoni Marekani anayesakwa na Uturuki kulingana na aliyekuwa
mkurugenzi wa idara ya ujajusi James Woolsey.
Uturuki inamshtumu kiongozi huyo wa dini Fethullah Gulen kwa kuandaa mapenduzi ya mwaka uliopita nchini Uturuki.
Katika mahojiano yalirekodiwa katika kanda ya video Bwana Woolsey aliambia jarida la Street Jaournal alikuwa katika mazungumzo kuhusu njia za kumuondoa kiongozi mbali na hatua halali za kisheria.
Hatahivyo Bwana Flynn amekana madai hayo ya Whoolsey.
Mkutano huo ulifanyika mnamo mwezi Septemba katika hoteli moja mjini New York.
Wale waliohudhuria mazungumzo hayo ni pamoja Flynn wakati huo akiwa mshauri wa bwana kampeni ya bwana Trump kuhusu maswala ya kiusalama, mwana wa kambo wa rais wa Uturuki Tayyip Erdogan pamoja na waziri wa maswala ya kigeni nchini Uturuki Mevlut Cavusoglu kulingana na jarida la Wall Street Journal.

Bunge nchini Benin limekuwa likifanya mjadala kuhusu marekebisho ya
katiba ikiwemo kupunguza muda wa rais kuongoza hadi muhula mmoja wa
miaka sita.
Kwa sasa rais anaweza kuongoza kwa mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja.
Lakini pendekezo hilo linakabiliwa na utata.
Vuguvugu moja la upinzani lilifanya mgomo mbele ya bunge likisema kuwa raia wanafaa kupewa fursa ya kujadili mabadiliko hayo.
Nchini Benin marekebisho ya kikatiba yanaweza kuidhinishwa kupitia kura ya maoni ama wingi wa kura bungeni.
Rais wa taifa hilo Patrice Talon alisema kuwa atajaribu kubadili katiba hiyo wakati wa kampeni ya uchaguzi mwaka uliopita.

Jumanne, 21 Machi 2017
@PerfectMaterial Music Inakulete @Shamsilatz na @Ramseetz wakisindikizwa na @Bullet_MtotowaGun pamoja na#KANGAMOKOInyeGwedegwede Tarehe 1-April Pale #IceAgeClub Usa River
Poster Imetengenezwa na @Will.I.Am.Art wa @LittleArushaCreations
Jumatatu, 20 Machi 2017
Jumapili, 19 Machi 2017
kwanza naanza kwa kumpongeza mkuu wa mkoa Rc makonda kiuhalisia/ kibinadam haiwezekani mtu akakuzalilisha watu na media zikaunga mkondo kwa uzalilishwaji kwako alafu wewe ukatoa ushahidi wa kitu husika media hizohizo zikakataa kucheza, safi sana Rc paul makonda kwa ulichowafanyia shilawadu nahisi wamepata fundisho na wengine
picha paul makonda
RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU::
Makonda alikuwa ofisi za Clouds mapema kuliko kawaida yake, mpaka tukahoji jamaa ana kipindi Clouds nini maana si kwa kuja huko kila siku lakini tuitetea tukajua ni sawa kama viongozi wengine wanavyofikaga mjengoni kila siku maana nikawaida yao!
Cha ajabu siku hiyo alikaa mpaka usiku akawa anamtafuta soudy Brown na Qwisser wa SHILAWADU muda huo walikuwa bado hawajafika kazini basi akawa anazungukazunguka tu ofisi hii anatokea ile kama mfanyakazi wa Clouds.
Kwenye Mida ya Saa kumi hivi akakutana na kina Soudy pamoja na prodyuza wa kipindi wakawa wanaongea kwa uficho hivi na usiri tukajua tu ni mambo ya kawaida ya kuhitaji uprivate lakini siku ile ulikuwa unatia mashaka sana.
Kumbe Makonda alikuja na Story ya mwanamke mmoja ambaye yeye Makonda alisema huyo mwanamke amezaa na mchungaji Gwajima na ametelekeza akawa anataka arekodiwe na ubuyu uruke kwenye kipindi cha SHILAWADU.
Basi wakakubalia kwa kuwa ni habari itabidi huyo mwanamke arekodiwe na kipindi kiruke siku ya jana lakini kawaida ya Kipindi cha SHILAWADU ubuyu ukipatikana lazima kila mtu apewe Natural Justice ya kusikilizwa pande zote mbili sababu huwa ndiyo kawaida ya kipindi.
Makonda siku hiyo hiyo ya Alhamisi akamwambia Soudy ajiandae then huyo mwanamke mnayemuona kwenye video na mtoto aliletwa na wasaidizi wa Makonda ahojiwe na Soudy Brown tayari kwa kurushwa kwa kipindi.
Siku ya Ijumaa ambayo ilikuwa ni jana SHILAWADU wakamtafuta Gwajima kwa upande wake kama anaifahamu hiyo ishu na je mwanamke huyo aliyetajwa ni kweli kwasababu tunaelewa ugomvi uliopo kati ya Makonda na Gwajima isijekuwa SHILAWADU wanatumika kuwafitinisha watu vibaya!
kwa bahati mbaya Gwajima hakupatikana jana ijumaa kwa ajili ya kurekodiwa na kufanyiwa mahojiano.
SHILAWADU wakatumia busara mpaka apatikane Gwajima scene ya Dada mwenye mtoto ziende kwa pamoja na ya mchungaji Gwajima kama kawaida ya POVU inavyokuwaga.
Jana usiku sasa kumbe Makonda alikuwa anafuatilia kipindi cha SHILAWADU aone kama kile kipande kitaruka hewani wapi ndiyo akaamua kuja Clouds na magari mawili yeye mwenyewe Makonda na Watu kama nane hivi wakiwa na Bunduki aina ya SMG geti la kawaida mlinzi alifungua geti kwasababu amezoeleka Mh anakujaga mjengoni wakafunguliwa kisha wakaingia ndani.
Walipofika reception wakazuiwa kuingia ndani sababu hatuna utaratibu wa kuruhusu wageni baada ya saa Nne usiku kuingia ndani ya Ofisi kama siyo mfanyakazi wa CLOUDS.
Alipoona wanazuiwa wakatoa bunduki zao mlinzi akashurutishwa afungue mlango kwa nguvu sababu walimtishia na Silaha mlimzi akafungua mlango wakaenda naye hadi studio kipindi kilikuwa kinaendelea hewani.
Makonda akawatoa nje Soudy na Mwenzake Qwisser akawauliza kwanini video aliyowaletea haijachezwa wakaelezea utaratibu jinsi utaratibu ulivyokuwa Qwisser wakati anajielezea akapigwa mtama akaanguka chini wakavamia mitambo ya transmission kwenye traycaster wakitaka kile kipande kirushwe hewani prodyuza wa kipindi akamuambia Makonda kwanini anavunja utaratibu na kutumia nguvu na ameshapewa utaratibu akapigwa na kitako cha Bunduki mgongoni akaanguka chini bahati mbaya kipindi kilikuwa kimefika mwisho.
Wakamshurutisha Prodyuza wa SHILAWADU anaitwa Chriss awape kile kipande wakaondoka naye wakati wanaondoka Ruge alikuja na Polisi akaingia lakini tayari walikuwa wameondoka ofisini wamechukua hicho kipande cha Video ya huyo mwanamke.
Hizo video zilichukuliwa kwa nguvu na Makonda na hao watu waliokuwa na Silaha inasemekana Makonda ana timu yake wanazisambaza kwa kasi na hatujui lengo lake ni nini.
Hata mkihitaji footage za Camera zipo jinsi tukio lilivyokuwa usiku wa jana.
By MANKA MUSA
JF-Expert Member
Source JF

Jumatatu, 13 Machi 2017
Alhamisi, 9 Machi 2017
Maafisa wa Marekani wamepinga pendekezo kwamba Korea Kaskazini itasitisha majaribio ya makombora yake na yale ya Kinyuklia iwapo Marekani itasitisha vitendo vyake katika eneo hilo.
Idara ya maswala ya kigeni nchini humo imesema kuwa mpango huo hautasaidia huku balozi wa Umoja wa Mataifa akisema kuwa Korea Kaskazini haifikirii.
Pendekezo hilo la China linajiri baada ya Korea kaskazini kufanya majaribio ya makombora yake manne ikiwa ni ukiukaji wa vikwazo vya kimataifa.
Wakati huohuo, Marekani imeanza kupeleka mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora nchini Korea Kusini.
Pia inaendela na mazoezi ya pamoja na wanajeshi wa Korea Kusini hatua inayokasirisha Korea kaskazini.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini China Wang Yi alisema siku ya Jumatano kwamba hali hiyo ni sawa na treni mbili zinazokaribiana kugongana ana kwa ana baada ya moja kati yazo kukataa kuipisha nyengine.
Usitishwaji wa operesheni za kijeshi na pande zote mbili unaweza kupunguza hali ya wasiwasi na kufungua mazungumzo alisema.
Lakini msemaji wa idara ya maswala ya kigeni nchini Marekani Mark Toner alisema kuwa hilo ni sawa na kufananisha ''tufaa na chungwa''.
''Kile tunachofanya kama ushirikiano wetu kujilinda na Korea Kusini ni tofauti na ukiukaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na Korea Kaskazini''.
Lakini amesema kuwa Marekani inafaa kuangalia mbinu nyengine za kukabiliana na Korea kaskazini.
''Juhudi zote tulizofanya kujaribu kulishawishi taifa la Korea Kaskazini kufanya majadiliano zimegonga mwamba.
''Kwa hivyo tunafaa kuangalia mbinu mpya za kulishawishi taifa hilo kuona kwamba ndilo litalalofaidika''.
Jumatatu, 6 Machi 2017
Mkurugenzi wa shirika la kijasusi la FBI James Comey amekana madai ya rais Donald Trump kwamba aliyekuwa rais wa taifa hilo Barrack Obama alidukua simu yake kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Bwana Comey amesema kuwa amelitaka shirika la haki nchini humo kukataa madai hayo kwamba Obama aliagiza uchunguzi wa simu za Donald Trump wakati wa kampeni za uchaguzi uliokwisha.
Alikana madai hayo akisema kuwa yanayoonyesha FBI ilivunja sheria.
Hatua hiyo iliripotiwa na gazeti la the New York Times na kuthibitishwa na NBC.
Idara ya haki haikutoa taarifa ya mara moja kuhusu ombi la bwana Comey.
Vyombo vya habari nchini Marekani viliwanukuu maafisa vikisema kuwa bwana Comey anaamini hakukuwa na ushahidi kuthibitisha madai ya Trump.
Rais huyo wa chama cha Republican ambaye anakabiliwa na uchunguzi mkali kuhusu uingiliaji wa Urusi ili kuunga mkono uchaguzi wake hajatoa ushahidi wowote kuunga mkono madai yake kwamba simu zake katika ofisi ya Trump Tower zilidukuliwa.
Jumapili, 5 Machi 2017
Jeshi la Korea kusini limesema Korea kaskazini imerusha makombora yake kadhaa katika bahari ya Japan, Jeshi la Korea kusini limesema kuwa makombora hayo yamerushwa kutoka kwenye eneo la Tongchang-ri lililo kwenye mpaka kati ya Korea kaskazini na China na kurushwa kwa umbali takriban kilomita elfu moja.
Akiongea na waandishi wa habari, waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema makombora hayo yanadhihirisha ushaidi tosha wa vitisho vipya kutoka kwa Korea kaskazini
''Korea kaskazini imefyatua makombora yake manne leo na kuangukia karibu na eneo letu la maji lenye manufaa kwetu kiuchumi.Japan itakusanya taarifa na kuzichambua kuhusu tukio hili.Japan inaipinga vikali Korea kaskazini.makombora yaliyorushwa wakati huu inaonyesha wazi kuwa Korea kaskazini ni tishio jipya.Korea kaskazini ilishatangaza aina hii mpya ya makombora kabla ya kuyarusha leo hivyo, tutafuatilia kwa karibu suala hili kwa kwa umakini mkubwa''
Katika kupambana na vita ya madawa ya kulevya inahitaji moyo wa kujitoa muhanga na hii vita siyo ya kupigana nayo mtu mmoja ( Individual attack) Kwani suala la madawa ya kulevya ni biashara ya kidunia (global trade). Kuna nchi kubwa Kama Mexico, Marekani, China nk zimejaribu kupambana na Biashara hii haramu inayoangamiza vijana wengi nchini mwao still wameshindwa, tena hapo wametumia mifumo imara ya kidola na sheria kali za kuwanyonga wote wanaobainika kuwa na madawa ya kulevya.
Binafsi navyoona Makonda angefanikiwa hii vita endapo tu angetumia njia sahihi kupigana vita hii. Toka awali alipoanza kutangaza majina nilionao tayari anavyoharibu strategy nzima ya kupambana na vita ya aina hii Kwani njia aliyoitumia (approach) ilikuwa siyo nzuri kuweza kuwakamata wahusika Wakuu wa madawa tofauti na kuwabaini tu wale wauzani. Narudia tena NI VIGUMU MNO Mh KUFANIKISHA VITA HII KWA APPROACH ALIYOITUMIA YA KUTAJA HADHARANI MAJINA YA WAHUSIKA Kwani kisheria sijuhi Kama inakubalika (watatusaidia wataalam wa sheria). Na hili afanikiwe basi anahitaji kuungwa mkono na Vyombo vya dola vyote pamoja na wananchi wanaochukia madawa ya kulevya (pamoja na mimi). Ila pia namshukuru kwa kuwa na moyo wa ujasiri kwa kuweza kujaribu hata kuingia ulingo wa kupigana hii vita Kwani siyo rahisi kutokana na kwamba hii biashara inafanywa na watu wenye uwezo kifedha (Capitalists) nchini na duniani kote.
Binafsi navyoona Makonda angefanikiwa hii vita endapo tu angetumia njia sahihi kupigana vita hii. Toka awali alipoanza kutangaza majina nilionao tayari anavyoharibu strategy nzima ya kupambana na vita ya aina hii Kwani njia aliyoitumia (approach) ilikuwa siyo nzuri kuweza kuwakamata wahusika Wakuu wa madawa tofauti na kuwabaini tu wale wauzaji wadogo na watumiaji Kama akina Chidz . Narudia tena NI VIGUMU MNO Mh KUFANIKISHA VITA HII KWA APPROACH ALIYOITUMIA YA KUTAJA HADHARANI MAJINA YA WAHUSIKA Kwani kisheria sijuhi Kama inakubalika (watatusaidia wataalam wa sheria). Na hili afanikiwe basi anahitaji kuungwa mkono na Vyombo vya dola vyote pamoja na wananchi wanaochukia madawa ya kulevya (pamoja na mimi). Ila pia namshukuru kwa kuwa na moyo wa ujasiri kwa kuweza kujaribu hata kuingia ulingo wa kupigana hii vita. Siyo kazi rahisi kazi nyepesi vile kutokana na kwamba hii biashara inafanywa na watu wenye uwezo kifedha (Capitalists) nchini na duniani kote. Zaidi tumwombee tu aweze kuendelea kupigana vita hii huku akitumia njia sahihi kwa kushirikiana na mamlaka husika ikiwamo tume/idara ya kupambana na madawa ya kulevya iliyoteuliwa na Mh Rais Magufuli.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameshiriki ibada na waumini wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ‘KKKT’ usharika wa Kimara Dar es salaam ambapo alipata nafasi ya kuzungumza mambo mbalimbali ikiwemo vita ya dawa za kulevya, Bonyeza play hapa chini nimekuwekea Full Video ya alichokizungumza.
Mexico imefungua vituo vya kutoa msaada wa kisheria katika balozi zake katika miji 50 ya Marekani, ili kulinda raia wake kutokana na utekelezaji mkali wa sheria za uhamiaji nchini humo.
Wakati wa ziara ya maafisa wakuu wa Marekani nchini Mexico mwezi uliyopita, utawala wa nchi hiyo ulielezea wasiwasi wake juu ya sera ya Trump ya uhamiaji dhidi ya raia wake.
Vituo hivyo vipya vitatoa msaada wa sheriak wa raia wa Mexico ambao wanahisi kuwa haki zao ziko hatarini nchini Marekani.
Uhusiano kati ya Mexico na Marekani umekuwa mbaya zaidi tangu miango kadha iliyopita.
Wiki moja baada ya kuapishwa mwezi Januari , Rais Donald Trump alisema kuwa atajenga ukuta kati ya mpaka wa Mexico na Marekani.
Alisisitiza kuwa Mexico italipia gharama ya ujenzi wa ukuta huo.
Matamshi hayo yalisababisha rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, kufuta safari yake nchini Marekania tarehe 31 mwezi Januari. na kutangaza ufadhili zaidi kulinda haki za za raia wa Mexico walio nchini Marekani.
Jeshi la Kenya
Vikosi vya Jeshi la Kenya vimewaua wapiganaji wa al-Shabaab 57 katika mapambano karibu na Afmadow, Somalia Alhamisi.
Saa 8.45 asubuhi mapigano yalizuka kama kilometa 31 kutoka Afmadow, mahali ambako majeshi ya Kenya yameweka kambi yao.
Msemaji wa KDF Joseph Owouth amesema idadi isiyojulikana ya magaidi walinusurika huku wakiwa wamejeruhiwa.
Wanajeshi wa KDF ambao wanaendesha operesheni zao chini ya Jeshi la Muungano wa Afrika (Amison) walipambana na magaidi hao.
Kanali Owouth ameongeza kuwa magari ya mizigo iliyokuwa imesheheni silaha nzito na silaha ndogo ndogo zinazomilikiwa na al-Shabaab pia ziliangamizwa.
“Askari wa KDF wamekuwa macho katika ulinzi wao na wataendelea bila ya kusita kuwafuatilia magaidi kuhakikisha kuna amani na usalama nchini Kenya na kuendelea kuzisaidia operesheni za Amisom kwa ajili ya kuiimarisha Somalia,” amesema.
Wakati huo huo Polisi wa Kenya wamesema watu wenye silaha wameteka walimu watatu katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab mashariki mwa nchi hiyo ambako kuna wakimbizi zaidi ya 200,000 wa kisomali.
Ripoti iliotolewa na shirika la AFP leo imeeleza watu watatu waliokuwa na bastola waliteka nyara walimu watatu wa shule ya Udha katika eneo la Hagadera la kambi ya Dadaab.
Rais Barack Obama
Uongozi wa Rais Donald Trump bado haujatoa tamko kujibu kauli ya msemaji wa Rais mstaafu Barack Obama ikikanusha kwamba aliamrisha udukuzi wa simu za Trump wakati wa kampeni kabla ya uchaguzi wa Marekani, mwaka jana.
Msemaji wa Obama ametoa tamko baada ya Trump kutuma mlolongo wa ujumbe wa tweets Jumamosi asubuhi akidai kwamba Obama “ aliamuru simu zake zirikodiwe kwa siri katika Jengo la Trump” huko Mji wa New York kabla ya uchaguzi.
Msaidizi wa Obama amesema kwamba madai ya Trump yalikuwa “ kwa kifupi sikweli.”
Trump hakueleza chanzo cha madai yake, au kutoa ushahidi wowote kwamba kulikuwa na uthibitisho wowote wa kielektronikia, lakini akafananisha na udukuzi wa siri zake kama ule wa kashfa ya Watergate ambao hatimaye mwaka 1974 ulipelekea Rais wa zamani wa Marekani Richard Nixon kujiuzulu.
Kashfa hiyo ilianza na mlolongo wa “vitimbi vya kisiasa” vilivyokusudiwa dhidi ya chama cha demokratik ikiwa ni njama ya wafuasi wa Nixon, na ikachukua sura mpya baada ya maafisa wa White House kutoboa siri kuwa Nixon aliruhusu operesheni hiyo ya kufuatilia mazungumzo ya chama cha Demokratik ifanyike White House, na kurikodi mazungumzo ya simu zao nyingi.
Lakini hakuna afisa yoyote wa White House wakati wa Uongozi wa Obama “ aliyewahi kuingilia uchunguzi wowote ulioendeshwa na Idara ya Sheria,” amesema Kevin Lewis, msemaji wa rais mstaafu, akisisitiza kuwa katazo hilo ndio ilikuwa “amri ya msingi” katika utawala wa Obama.
Katika taarifa hiyo, Lewis amesema haikuwa Rais Obama wala afisa yoyote wa White House aliyewahi kuamrisha uchunguzi wa raia yoyote wa Marekani. Kauli yoyote inayopendekeza hilo ni Uongo tu.
VOA imewataka maafisa wa White House kutoa tamko kuhusu tukio hilo la Jumamosi lakini hawakuweza kupata majibu hayo mara moja. Sio Idara ya FBI wala Idara ya Sheria iliyoweza kutoa tamko kuhusiano na madai hayo.
Waziri mkuu wa Somalia Hassan ali Khaire, amesema watu mia moja na kumi wamefariki kutokana na visa vinavyo husiana na ukame na baa la njaa katika eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo, katika kipindi cha saa nane zilizopita.
Ukame mbaya unaokumba Somalia unatishia maisha wa mamilioni ya watu nchini humo.
Ukame mbaya unaokumba Somalia unatishia maisha wa mamilioni ya watu nchini humo.
Siku ya Jumanne Rais Mohamed Abdullahi Farmajo, alitangaza ukame huo kuwa janga la kitaifa.
Umoja wa Mataifa una kadiria watu milioni tano nchini Somalia, wanahitaji msaada wa dharura na kuongeza kuwa taifa hilo ni moja kati ya mataifa manne, yaliyo katika hatari ya kukumbwa na janga la njaa.
Mataifa mengine ni Nigeria, Sudan kusini na Yemen.
Karibu watu 260,000 walifariki kutokana na baa njaa iliyokumba Somalia kuanzia mwaka 2010 na 2012.
Watu wengine 220,000 walifariki kutokana na njaa ya mwaka 1992.
Jumamosi, 4 Machi 2017
Mamlaka nchini Guinea imesema kuwa kuna zaidi ya wanafunzi bandia 47,000 katika vyuo vikuu vya taifa hilo.
Takwimu hizo zilichapishwa siku ya Alhamisi na waziri wa elimu ya juu baada ya usajili wa kielektroniki.
Mpango huo uliwafutilia mbali wanafunzi hewa.
Mamlaka ya Guinea hutoa ruzuku kwa vyuo vikuu kulingana na idadi ya wanafunzi.
Waandishi wa habari wanasema vyuo vikuu vya umma vimejaa na ruzuku hizo hutolewa kushinikiza upanuzi katika vyuo vikuu vya kibinafsi.
Hatahivyo baadhi ya vyuo vya kibinafsi vimeongeza idadi bandia ya wanafunzi ili kupata ruzuku zaidi.
Hakuna tamko lolote la vile serikali itakavyokabiliana na madai hatua hiyo
Waandishi wawili wa Zimbabwe wamekamatwa kuhusiana na ripoti ya gazeti moja ilioelezea kwamba afya ya rais wa taifa hilo Robert Mugabe 'imedhoofika' alipoelekea nchini Singapore kwa kile afisi ya rais huyo ilisema ni zaira ya kimatibabu.
Muhariri wa gazeti la kibinafsi la NewsDay ,Wisdom Mudzungairi na mwandishi aliyeandika ripoti hiyo Richard Chidza hatahivyo wameachiliwa na ni sharti wajiwasilishe mahakamani.
Wakili wao Obey Shava amesema kuwa wameshtakiwa kwa kuhujumu na kutusi afisi ya rais.
Taarifa hiyo iliosema 'Mugabe yuko katika hali mbaya' ilinukuu duru zikisema kuwa rais huyo alisafirishwa kwa ndege siku ya Jumatano alfajiri.
Mugabe alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya mwaka 93 na amekuwa katika mamlaka tangu 1980.
Kulingana na chombo cha habari cha AP, watu wanaopatikana na hatia ya kumtusi Mugabe, uhudumia kifungo ijapokuwa kesi nyengine zimetupiliwa mbali.
Malaysia imemfukuza balozi wa Korea Kaskazini kuhusiana na kifo cha Kim Jong nam ,ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea kaskazini.
Kang Chol amepewa agizo la kuondoka nchini humo katika kipindi cha saa 48, alisema waziri wa maswala ya kigeni nchini humo.
Kim Jong nam ndugu wa kambo wa Kim Jong un ,alifariki wiki tatu baada ya wanawake 2 kumpaka kemikali ya sumu usoni mwake katika uwanja wa kuala Lumpur .
Malaysia haijailaumu Korea kaskazni kwa shambulio hilo lakini kuna shauku kwamba Pyongyang ilihusika.
Balozi wa Korea Kaskazini, Bwana Kang alitangazwa persona non grata{ hatakiwa nchini humo} siku ya Jumamosi baada ya kusema kuwa taifa lake haliweza kuamini uchunguzi uliofanywa na Malaysia na kwamba uchunguzi huo ulikuwa ukiingiliwa.
Waziri wa maswala ya kigeni wa Malaysia Anifah Aman alisema katika taarifa kwamba taifa lake linataka kuombwa msamaha na balozi huyo kwa matamashi yake lakini mwanadiplomasia huyo hakuomba msamaha.
''Malaysia itajibu matusi yoyote dhidi yake ama jaribio lolote la kutaka kuiharibia sifa'',alisema bwana Anifah.
Malaysia ni miongoni mwa mataifa machache yaliokuwa na urafiki na Korea Kaskazini.
Rais wa Marekani Donald Trump amemshutumu mtangulizi wake kwa kudukua simu yake mwezi mmoja kabla ya kuchaguliwa kuliongoza taifa hilo.
Rais Trump alichapisha ujumbe wa Twitter mapema siku ya Jumamosi akisema: Makosa sana! Nimegundua kwamba rais Obama alikuwa akidukua simu yangu katika afisi yangu iliopo Trump Tower kabla ya mimi kupata ushindi .

Aliongezea kwamba awali mahakama moja ilipinga uchunguzi kuhusu kudukuliwa kwa simu yake.
Rais huyo wa Marekani hajatoa ushahidi wowote ili kuthibitisha madai hayo ama hata kusema ni agizo gani la mahakama alilonukuu.
Ripoti za vyombo vya habari zimesema kuwa shirika la kijasusi la FBI liliomba agizo la kuwachunguza maafisa wa karibu wa Rais Trump kutoka kwa shirika la kigeni la kijasusi Fisa kubaini iwapo wamekuwa wakiwasiliana na maafisa wa Urusi.
Agizo hilo lilikataliwa lakini baadaye likakubaliwa mwezo Oktoba kulingana na ripoti hizo za vyombo vya habari.
Hakujakuwa na thibtisho rasmi na pia haijulikani iwapo hatua hiyo ilichunguzwa.