Najua kuna watu wangu ni mashabiki wa staa wa muziki wa RnB na Pop mwenye asili ya Canada, Justin Bieber amezikamata headlines baada ya kutupa mic chini akiwa anaperfom kwenye stage za show ya Manchester usiku wa Oct 23 2016 na kuondoka jukwaani hapo.
Imetajwa na kituo kikubwa cha habari cha Enews cha Marekani
kuwa mashabiki kwenye show hiyo walikuwa wakipiga kelele za shangwe
kupita kiasi na kumkera staa huyo ambapo alidai kuwa anataka aongee nao
badala yake zinasikika kelele ndipo akamua kuchukua uwamuzi huo.
Enews
waliongezea kuwa Justin alishawaonya mara ya kwanza mashabiki wasipige
kelele wakati anaongea nao lakini hawakusikia na haya ndiyo yalikuwa
maneno ya Justin…..
>>>’Nashukuru
sana kwa upendo wenu mnao uonyesha kwangu, hizi kelele tafadhali naomba
ziachwe ninashukuru tena lakini sidhani kama ni lazima kwenu
kushangilia wakati naongea kwasababu najisikia kama nataka kuunganishwa
na ninyi’ –Justin Bieber
Nimekuwekea hapa chini video mtu wangu jinsi Justin alivyotupa Mic nakuondoka kwenye stage hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni