Utoaji wa tuzo za MTV Mama 2016 zinazoandaliwa na kituo cha TV cha MTV Base Africa ulikamilika usiku wa October 22 2016 Johannesburg Afrika Kusini, msanii wa Bongofleva Diamond Platnumz alikuwa ni mmoja kati ya wasanii wa Tanzania waliokuwa nominated kuwania tuzo hizo.
Diamond alikuwa kateuliwa kuwania tuzo mbili za msanii bora wa mwaka na msanii bora wa kiume, tuzo ambazo zote alishinda Wizkid wa Nigeria, muda mchache baada ya tuzo kumalizika Diamond Platnumz alitumia account yake ya Instagram kuwashukuru wote na kuwapongeza washindi akioneshwa kukubali matokeo.
“Shukran
sana sana kwa Kura na support Kubwa mlionipa na mnayoendelea kunipa….
pia S/O kwa my fellow Tanzanian Artist wote waliobahatika kuchaguliwa…
Kuingia tunwengi kwenye MtvAwards ni Ushindi tosha kwa Tanzania…ila wanna congrats my brothers @sautisol for the Best Group award… my hommie @jahprayzah and@wizkidayo ya’ll deserve the Trophies…. ”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni