mo dadyTV

KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

kARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

LightBlog
KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

Karibu kutangaza nasi mawasiliano 0652231836

Jumapili, 23 Oktoba 2016

AY,Diamond,Harmonize na Dj D Ommy washinda tuzo za AEA za Marekani.

Wakati Watanzania wengi macho na masikio yetu tukiwa tumeyaelekeza kwenye utoaji wa tuzo za MTVMama ambazo zimetolewa Afrika Kusini lakini usiku huo huo wa Oct 22 kuamkia Oct 23 nchini Marekani kulikua pia kukitolewa tuzo ambazo Watanzania wenzetu pia walishiriki.
 Tuzo ambazo zilitolewa marekani zinajulikana kama African Entertainment Awards Usa 2016 (AEA) kitu kizuri na kikubwa ni kwamba Watanzania wenzetu wameshinda pia kwenye tuzo hizo kwenye baadhi ya vipengele.
Kipengele cha Msanii bora anaechipukia kashinda Harmonize,Kipengele cha wimbo bora wa kushirikiana/kushirikishwa umeshinda wimbo wa Zigo wa AY,Kipengele cha DJ Bora ni Dj D Ommy na msanii bora wa kiume kashinda Diamond Platnumz.
Tuzo aliyoshinda Harmonize alikua anashindana na Tekno Miles,Ziza Bafana,Ayo Jay,Missy Bk,Jay Oliver,Den G,Togar  Howard na Ziza Bafana.Tuzo aliyoshinda AY wimbo bora wa kushirikiana alikua akishinda na Nagharamia ya Christian Bella na Alikiba,Woju ya Kiss Daniel akiwa kamshirikisha Davido na Tiwa Savage,Pimpina ya Obrafour akiwa kamshrikisha Bisa Kdei,Porque te amo ya To Semedo akiwa kamshirikisha Boss Ac na wimbo wa Nagode wa Yemi Alade akiwa kamshirikisha Selebobo.
Tuzo aliyoshinda Dj D Ommy alikua akishinda na Dj Tunez,Dj Van,Dj Mensah,Dj Brazao,Dj BossMan na Dj Jimmy Jatt,tuzo ya msanii bora wa kiume aliyoshinda Diamond kipengele hicho alikua na Eddy Kenzo,Wizkid,Mc Galaxy,Nelson freitas,Coreon Du na Master jake.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni