mo dadyTV

KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

kARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

LightBlog
KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

Karibu kutangaza nasi mawasiliano 0652231836

Alhamisi, 20 Oktoba 2016

BREAKING NEWS

Serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam, imewataka wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutosaini fedha za malipo ya mkopo wa kujikimu hadi hapo serikali itakapokuja na majibu.

Rais wa serikali hiyo Erasmi Leon, akitoa msimamo wa Serikali ya wanafunzi wa UDSM amesema wanapinga mfumo mpya wa HESLB ambao unawapa mkopo wanafunzi kulingana na daraja na kwamba wanafunzi wa mwaka wa kwanza hawatasaini fedha hizo mpaka pale kasoro hiyo itakaporekebishwa.

Imebainika kwamba,utaratibu mpya wa kutoa fedha za kujikimu kwa mwanafunzi kulingana na asilimia ya mkopo, ulioanzishwa na serikali mwaka huu wa masomo,umesababisha baadhi ya wanafunzi kupewa Sh. 350/= kama fedha ya kujikimu kwa siku, tofauti na mwaka jana ambapo wanafunzi wote wenye mikopo walikuwa wakipewa Sh. 8,500/= kwa siku.

Erasmi amesema wana kila sababu ya kusikilizwa na wakinyimwa nafasi watachukua hatua nyingine zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni