Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe amelaani vikali tabia ya wakuu wa wilaya na mikoa nchini kuingilia mamlaka zisizo zao.
Kiongozi huyo alikuwa alikuwa
akizungumza na wanahabari mjini Arusha mara baada ya kuhudhuria kesi ya
Rufaa ya aliyekuwa mbunge wa Longido Onesmo Ole Nangole.
Kiongozi huyo wa upinzani bungeni
ameonya na kulaani tabia ya mkuu wa mkoa wa Arusha akishirikiana na
wakuu wake wa wilaya kudhalilisha madiwani wa Chadema bila sababu.
Mwenyekiti huyo amesema viongozi hao wa
kuteuliwa wamekuwa wakitengua maamuzi ya vikao halali vya mabaraza vya
madiwani kihuni na bila sababu za msingi ati kwa vile tu mabaraza hayo
yanaongozwa na Chadema.
Mwenyekiti huyo amesema posho ambazo
zinalipwa madiwani zilipitishwa na Baraza la madiwani wa CCM wakitaka
kubadilisha posho hizo Mkuregenzi wa Jiji la Arusha anatakiwa kuwapatia
madiwani waraka unatakiwa kutoka ofisi ya Tamisemi.
Kiongozi huyo mkuu wa upinzani nchini
ameagiza wanasheria wa chama kuchukua hatua mara moja dhidi ya wakuu wa
mikoa na wilaya wanaofanya vitendo vinavyokiuka maadili ya kazi zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni