Mabingwa wa soka barani Ulaya klabu ya Real Madrid wamechupa hadi
katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi ya nchini Hispania baada
ya kuchomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Athletic
Bilbao.
Karim Benzema alitangulia kuzisalimia nyavu za Bilbao katika 7, lakini dakika 19 baadae Sabin Merino aliisawazishia timu yake ambayo ilikua ugenini Santiago Beranabeu usiku wa kuamkia hii leo.
Alvaro Morata, ambaye jana alikua akisheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kufikisha umri wa miaka 24 alifunga bao la ushindi kwa Real Madrid katika dakika ya 84.
Kwa ushindi huo Real Madrid wamekwea katika kilele cha msimamo wa ligi ya La Liga kwa kufikisha point 21, wakifuatiwa na Sevilla CF wenye point 20 na nafasi ya tatu ikishi FC Barcelona wenye point 19.
Michezo mingine ya ligi hiyo iliyochezwa jana:
Celta Vigo 4 – 1 Deportivo La Coruna
Sevilla 1 – 0 Atletico Madrid
Malaga 4 – 0 Leganes
Villarreal 2 – 1 Las Palmas

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni