Rais wa Makampuni *CNBM* kutoka Beijing CHINA *Bw. Cao Jiang Lin*
amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe
Paul Makonda,* jiji Dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo, *Bw. Lin* amemuhakikisha mkuu wa mkoa *Mhe Makonda* kuwa makampuni mengi yameonyesha nia ya dhati ya kuja kuwekeza *Tanzania* na Dar es salaam ambapo tayari baadhi ya makampuni yameshaanza kuwekeza jijini *Dar es salaam.*
Katika Mazungumzo yao, *Bw. Lin* amemuahidi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe Makonda* kuwapatia *kazi vijana wa Dar es salaam zaidi ya 500* kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Ikumbukwe makampuni ya *CNBM* yako zaidi ya *500 duniani* na ndiyo makampuni yanayoongoza kwa uzalishaji wa cement na bidhaa zaidi ya *15,000 DUNIANI.*
*Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.*
*27/05/2017*

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni