mo dadyTV

KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

kARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

LightBlog
KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

Karibu kutangaza nasi mawasiliano 0652231836

Jumapili, 21 Mei 2017

Ni kama ligi ya mawaziri wa kale na wapya



Bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma limeghubikwa na mijadala mingi na ya kusisimua ikihusisha hoja nzito zinazotoka kambi za upinzani na CCM, huku pia mawaziri wa kale na wapya wakionekana kana kwamba wana ‘ligi’ yao.

Wakati aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ‘akipambana’ na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge alipochangia kuhusu suala la maji jimboni kwake, Waziri wa zamani wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye alionyesha msuli wake katika suala maji jimboni kwake.

Kitwanga alieleza kuwa yale aliyochangia kwenye bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji bungeni ni kama ali-‘beep’ ila mazito yanakuja.
Hata hivyo, Lwenge alimjibu Kitwanga kuwa kama haoni mambo Serikali ilifanya katika wilaya yake ajiondoe katika chama hicho.
“Sasa anaposema anakwenda kuhamasisha wananchi wakabomoe mtambo wa Ihelele maana yake analeta uasi au hathamini kazi iliyofanywa na chama chake,” alisema.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni