mo dadyTV

KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

kARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

LightBlog
KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

Karibu kutangaza nasi mawasiliano 0652231836

Jumapili, 7 Mei 2017

CCM YAANDAA VIJANA KUWA VIONGOZI WA BAADAE

Chama tawala nchini Tanzania kinachoitwa Chama cha mapinduzi (CCM) huwa kina kawaida ya kipekee Barani Afrika kwa kutengeneza viongozi watakao kuja kutawala nchini humo na viongozi hao wanaoandaliwa kwa ajili ya kuja kuongoza baadae ni vijana
vijana wa ccm
Vijana hao hukuzwa kwa nidhamu ukakamavu na uwadilifu.. 
Tamaduni hii ya kuandaa vijana kuwa viongozi ni yakipekee kabisa balani Afrika na hata nchini Tanzania mmoja kati ya vijana ambao waliandaliwa vyema kuja kuwa kiongozi wa Tanzania ni Rais mstafu wa Awamu ya 4 Mh.Jakaya mlisho kikwete

Historia Fupi ya Rais mstaafu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Jakaya M. Kikwete


Asili.

Amezaliwa 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugobatarafa ya Msoga,jimbo la uchaguzi la ChalinzeWilaya ya Bagamoyomkoa wa Pwani.
Alizaliwa katika familia ya wanasiasaBabu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifuwa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya PanganiSame na Tanga.
Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwamja mzito naye, babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithiwa cheo chake.

Masomo

Miaka 1958 – 1961 akasoma Shule ya Msingi Msoga, halafu 1962 – 1965 Shule ya Kati (Middle School) Lusonga, halafu Shule ya Sekondari Kibaha akiongeza A-level huko Shule ya Sekondari Tanga.
Kuanzia mwaka 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaamakimaliza kwa kupata digrii yake mwaka 1978.
Akajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Jakaya aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzina pia wa Vijana wa TANU. Katika Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuuna pia kiongozi wa timu ya mpira. Katika UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wahalmashauri ya wanafunzi.

Kupanda ngazi katika siasa

1mwaka huu alikuwa mkulima wa Msoga. Mwaka 1988 akateuliwa kuwa mbunge nawaziri msaidizi. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/Chalinzeakirudishwa kila uchaguzi hadi mwaka 2000. Akawa waziri akipita katika wizara zamaji na fedha.
Mwaka 1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwalimu Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia nafasi Benjamin Mkapa aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawaWaziri wa Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa.
Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya rais akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za kura zote.
Kutokana na Historia Hii fupi Tunaona jinsi Rais mstafu Jakaya mrisho kikwete alivyo andaliwa vizuri kisiasa na kuja kuwa kiongozi mzuri wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania....
Napenda kushauli vyama pinzani au vyama vya kisiasa kufata mfumo huu wa kuandaa viongozi tangu wakiwa wadogo ili kuweza kuja kupata viongozi bora wa baadae

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni