Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi ameendelea na juhudi za utatuzi wa migogoro ya ardhi ambayo inahusisha wananchi wenye mashamba katika maeneo ya Kinondo, Dovya na Mbopo.
Juhudi hizo zimedhihirika Leo katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa kilichohusisha wananchi pamoja na wataalam wa Mipangomiji kwa kuwaahidi wananchi hao kumaliza mgogoro hiyo ili waweze kuishi kwa amani.
Hapi amesema dira ya Wilaya ya Kinondoni ni kuhakikisha viwanja vyote vinapimwa ili kuweka mipango mizuri ya matumizi ya Ardhi itakayozuia uvamizi wa mashamba pamoja na maeneo ya wazi.
Aidha amewataka wale wote wanaomiliki maeneo hayo kuyaendeleza baada ya kufanyiwa upimaji ili kuepusha migogoro ya mipaka inayoweza kutokea.
Migogoro mingine inayoendelea kutatuliwa ni pamoja na TBA Mabwepande na Nyakasangwe ambayo kwa sasa maeneo hayo yamefikia hatua ya upimaji viwanja.
Mkuu wa wilaya ya kinondoni Ally Hapi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni