Rais wa shirikisho la soka ulimwengu FIFA Gianni Infantino anapanga
kuboresha michuano ya klabu Bingwa dunia kutoka timu 7 hadi timu 32
lengo likiwa ni kuboresha michuano hiyo ili ilete mvuto tofauti na
ilivyokuwa sasa.
Gianni Infantino
ametoa wazo hilo na kutazamiwa lianze kufanyiwa kazi katika michuano ya
klabu Bingwa dunia kuanzia mwaka 2019, michuano hiyo kwa sasa
inashirikisha timu 7 kitu ambacho kinatajwa kutokuwa na mvuto na kufanya
mshindi iwe rahisi kumtabiri.
Rais huyo anaamini kubadili mfumo huo kutafanya kuongeza mvuto wa mashindano hayo, ambapo karibia kila mara Bingwa wa Ulaya na America Kusini ndio huwa wanakutana fainali, Infantino anaamini mashindano hayo yakiwa yanachezwa kuanzia June 10 hadi June 30 yakishirikisha timu 32 yatakuwa na mvuto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni