Kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji anayeichezea Chelsea ya London Eden Hazard
November 18 2016 alitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi
October, baada ya kucheza mechi nne, kufunga goli tatu na kutoa assist
katika ushindi wa Chelsea wa mechi zote nne.
Eden Hazard ambaye amekuwa akitajwa kuhitajika kwa miaka kadhaa sasa na klabu ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa na kuwa amekuwa akisisitiza kuwa na furaha katika klabu ya Chelsea, ameweka wazi kuwa anaweza kuondoka Chelsea ila ni baada ya kutwaa Ubingwa.
“Ndio
naweza kuondoka Chelsea siku moja lakini ni baada ya kuisaidia kutwaa
Ubingwa, unahitaji kucheza vizuri na kwa kujitoa ili watu waweze
kukukumbuka kwa sababu za msingi”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni