mo dadyTV

KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

kARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

LightBlog
KARIBU KUTANGAZA NASI 0652231836

Karibu kutangaza nasi mawasiliano 0652231836

Jumapili, 13 Oktoba 2024

 Body ya wamata mkoa wa pwani kupitia katibu wake Chriss kyando mnano tar 07.09.2024 ilikuwa katika wilaya ya kibiti mkoan pwani kwajili ya uzinduzi wa tawi la wamata katika kata ya imai wilaya ya kibiti 

Body iyo ya wamata mkoa wa pwani wakiwa na mwenyeji wao katibu wilaya ya kibiti waliongoza matukio mbali mbali ikiwemo matukio yakupanda miti katika shule ilio mpya ya wananchi


       Chriss kyando,katibu wamata kibiti.    Pia baadhi ya wananchi pamoja na walimu walipata bahati yakushiliki katika zoezi ilo la upandaji miti wakiungana na kiongozi uyo mkubwa wa wamata mkoa huo

                Mwananchi akipanga mti

Baada ya zoezi ilo la kushiliki zoezi la kijamii bodi hiyo ya mkoa wapwani ikiongozwa na katibu wake Chriss kyando ili ilekea katika kata ya imani kwajili ya uzinduzi wa tawi la imai kata ya kibiti 

Katibu uyo wa mkoa wa pwani aliwahasa wana imai kuongelea mambo mazuli ambay  Rais Samia ameweza kuyafanya ikiwemo miladi mikubwa ambayo raisi wa jamuuri ya muungano wa Tanzania ameweza kuyafanya mamengine mengi mazuri aliyo weza kuyafanya


         Pia diwani wa kata ya imai aliweza kuhutubia hadhala iyo


           Diwani IMAI WILAYA YA KIBITI






Jumatatu, 10 Julai 2017

Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema CCM, William Ngeleja ametangaza kurejesha pesa za ESCROW, kiasi cha Tsh. mil. 40.4 alizopokea kutoka kwa James Rugemalira anayetuhumiwa katika sakata la ESCROW tarehe 12 Februari 2014. Ngeleja amewaambia wanahabari leo kuwa,tayari amerudisha TRA TSh 40.4milioni alizokuwa amepewa na mfanyabiashara James Rugemalila.

Jumatatu, 26 Juni 2017

Producer bora toka Arusha aliewai kuproduce hit song nying ikiwemo nishuke wapi ya real voice inasemekana kudaiwa kuachana na mpenzi wake aliekuwa akijulikana kwa jina la Johari na sasa hupo katika wimbi la mapenzi mazito na kigori mmoja huko arusha ambaye atukuweza kumjua jina Wawili hao wamekuwa wakioneka sehemu mbalimbali za bata...
Mo fravour
Blog yetu inaendelea kunafanya juhudi za kumtafuta Johari ili atusibitishie ameachana na Mo Flavour au la



Ijumaa, 23 Juni 2017

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amelazimika kula chakula na kunywa maji yaliyotoka kwenye mradi wa maji wa kisima kirefu uliokataliwa na wananchi kwa hofu kuwa wakinywa maji hayo watakufa na wakipikia chakula kitabadilika rangi ya njano.
Mkuu huyo akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji hicho juzi alitaka kusikiliza kero za wananchi na kufahamu kwanini wanaendelea kutumia maji ambayo siyo safi na salama ikiwa mradi upo tangu mwaka 2014 hawajawahi kuyatumia.
Matiro aliyekuwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama na viongozi wengine na baada ya kusikiliza hoja hiyo walilazimika kuyaonja na kupika chakula kwa haraka na kubainika hayana chumvi wala chakula kilichopikwa kutokuwa cha njano ndipo ilipobainika kuwa walidanganywa kwa sababu za kisiasa.

Jumatatu, 19 Juni 2017

WATANZANIA wametakiwa kutoa taarifa wanabaini uwepo wa mchele usioeleweka, baada ya kuibuka kwa taarifa ya mchele bandia wa plastiki kukamatwa Nigeria.
Msemaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudencia Simwanza alisema hayo jana .
Alisema wao sasa wana mifumo mizuri ya kudhibiti uingizwaji wa bidhaa zisizofaa na mpaka sasa mfumo huo haujabaini mchele wa aina hiyo nchini.
"Tunadhibiti na tuko makini kufuatilia wafanyabiashara wanaoingiza vitu haramu na kama huo mchele ungekuwa umeingia, tungeshajua," alisema.
Mwandishi wa habari hii alipomwuliza ikitokea umeingizwa kimagendo nchini, Watamzania watautambua vipi, Gaudencia aliwataka kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa watakapoona mchele wasiouelewa.
Mchele huo bandia ulikamatwa na Mamlaka ya Mji wa Lagos, Nigeria wiki hii, ambapo walikamata magunia 102.
Taarifa kutoka nchini humo, zilieleza kuwa uliingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu na unafanana na mchele wa kawaida, hivyo ni ngumu kuutofautisha na mchele wa kawaida.
Kutokana na kusambaa kwa kasi kwa mchele huo, huwezi kuutambua kwa haraka hadi pale unapopikwa ndipo unaweza kuona ni mchele wa plastiki. Hata hivyo baadhi ya wataalamu walisema kabla ya kuupika mchele huo ukilowekwa kwenye chombo chenye maji unaelea tofauti na halisi ambao huzama.