Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema CCM,
William Ngeleja ametangaza kurejesha pesa za ESCROW, kiasi cha Tsh. mil.
40.4 alizopokea kutoka kwa James Rugemalira anayetuhumiwa katika sakata
la ESCROW tarehe 12 Februari 2014. Ngeleja amewaambia wanahabari leo
kuwa,tayari amerudisha TRA TSh 40.4milioni alizokuwa amepewa na
mfanyabiashara James Rugemalila.